Kamati Kuu ya Chadema Kukutana Leo

Kamati Kuu ya Chadema Kukutana Leo
Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema Leo Jumamosi January 13, kinatakiwa kufanya kikao cha Kamati Kuu ya Chama.

Kikao hicho kimekuja siku tatu tangu mmoja wa wajumbe wake, Edward Lowassa kufanye ziara Ikulu na kuzungumza na Rais John Magufuli kitendo ambacho kilisababisha mvutano ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Bila shaka, kikao cha leo kitakachokuwa chini ya uenyekiti wa Freeman Mbowe, mbali na mambo mengine kitataka kujua undani wa mazungumzo ya mjumbe huyo na Rais Magufuli.

Ingawa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu alisema jana kwamba kikao hicho kimeitishwa kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya kisiasa nchini, baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema suala la kikao cha Lowassa na Rais Ikulu linaweza kuwa na mjadala mpana zaidi katika kikao hicho.

Hata hivyo, Mwalimu alisema ajenda za kikao hicho zilipangwa kabla Waziri Mkuu huyo wa zamani hajaenda Ikulu hivyo hakina uhusiano na ziara hiyo ila huenda jambo hilo likajitokeza.

“Suala hilo halipo kwenye ajenda ila linaweza kujitokeza na likijitokeza litazungumziwa lisipojitokeza basi,” alisema Mwalimu na kuongeza;

“Hata hivyo, kwa upande wake inaweza kuwa fursa nzuri kuielezea Kamati Kuu na viongozi wenzake nini kilitokea.”

Alisisitiza kuwa kikao hicho si cha dharura kwani kilipangwa kufanyika Desemba mwaka jana lakini kiliahirishwa kutokana na sikukuu za mwisho wa mwaka.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad