Kamati ya Kuchunguza Madini ya Tanzanite Yaanza Kazi

Kamati ya Kuchunguza Madini ya Tanzanite Yaanza Kazi
Kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite imeanza kufanya mazungumzo na kampuni ya Tanzanite One.

Mwenyekiti wa kamati hiyo  Waziri wa Katiba na Sheria Profesa  Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo hayo yaliyoanza jana  Januari 16 , 2018 yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee.

Profesa Kabudi amesema mazungumzo yameanza vizuri ambapo pande hizo mbili zinapitia matatizo yote yanayohusu biashara ya madini ya Tanzanite, utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za madini na mapato ya rasilimali hiyo, ili hatimaye zikubaliane namna bora itakayohakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad