Kampuni ya mavazi, H&M imelazimika kufunga maduka yake kwa muda nchini Afrika Kusini baada ya kutokea uharibifu.
Hatua ya kufunga maduka hayo imekuja baada ya kundi la Economic Freedom Fighters (EFF) kuyalenga maduka takribani sita na kuyaharibu ikiwemo na bidhaa zake.
H&M wameachia taarifa ya kufunga maduka hayo kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Twitter, na kuelezea kuwa hatua hiyo imefanywa ili kulinda usalama wa wafanyakazi na wateja wao.
Wiki moja iliyopita kampuni hiyo ilichapisha T-Shirt iliyovaliwa na kijana mwenye asili ya Afrika na kuandikwa “Coolest monkey in the jungle”, kitendo hicho limetafrisiwa kuwa cha kibaguzi kwa watu weusi na kupelekea watu mbalimbali kulaani kampuni hiyo kwa kufanya kitendo hicho.
Kampuni ya mavazi, H&M Yafunga Maduka Yake Afrika Kusini
0
January 15, 2018
Tags