Wadau,
Katika mizunguko yangu ya kikazi kuna kitu nilikuwa nakiangalia hasa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Huu ni msimu wa kilimo, wakati nikiwa kwenye gari kuanzia kanda ya ziwa hadi Morogoro nimeona kuna pilikapilika nyingi za kilimo. Yaani kuanzia kanda ya Ziwa inaonekana green ya mahindi na mazao mengine.
Lakini maajabu ni kwamba wakati nikitokea Dar es salaam kuelekea Arusha, kuanzia Mlandizi karibu mto Ruvu hadi Segera, kila nikitizama kwenye vijiji vya pembeni nimekuwa nikiona green ya mapori tu.
Ukweli nimejiuliza sana, kwanini naona green ya mapori badala ya Mazao wakati huu ni msimu wa kilimo, au eneo hili ni hifadhi ya taifa? Nikajiuliza, hawa watu hawalimi, lakini pia hawafugi, je wanaishije?.
Lakini maajabu mengine ni kwamba eneo lote hili hasa Chalinze hadi Segera, nyumba asilimia kubwa ni za fito na tope (Mbavu za mbwa tunaita), yaani unakuta nyumba mbavu za mbwa iko katikati ya kijani cha pori lakini hakuna mazao wala maandalizi kwa ajili ya kilimo licha ya kwamba ni msimu wa mvua. Vijiji hivi vina umasikini wa kutupa, utajua kwa kutizama mbavu za mbwa zilizopo.
Ndugu zangu, vijana wenzangu mnaoishi maeneo hayo, mnarudisha taifa nyuma, kwanini hamtaki kutumia ukaribu wenu na Dar es salaam mkauza mazao mkabadilisha hali zenu za maisha? Kwanini wakulima wa Songea wanufaike na uuzaji wa mahindi Dar na nyie msitumie fursa ya ukaribu huo? Kwa tabia hii nina uhakika kila mwaka huwa mnaletewa mahindi ya njaa kutoka serikalini.
Nashauri, itungwe sheria ya kulazimisha watu kufanya kazi. Pia wabunge wa maeneo haya, hasa Ridhiwani na wengine, tafadhali hamasisha watu wako kufanya kazi.
By Nkobe