Baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kumtembelea Rais Magufuli Ikulu Leo January 9, 2018 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ametoa mtazamo wake kuhusu suala hilo
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lissu amepost picha inayomuonesha Lowassa akiwa Ikulu na kuandika maelezo haya; “Na hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili nchi yetu.”
“Lakini ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na washauriane kabla ya mazungumzo hayo. Na baada ya mazungumzo, ni lazima viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote tuwe kwenye ukurasa mmoja.
“Viongozi na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani kwa mapanga na hata kwa risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye. Katika mazingira ya kesi nyingi za kutunga dhidi yetu, ‘kazi nzuri’ inayofanywa ina maana gani, kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa.
“Katika mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa Rais Magufuli, kutoa kauli kwamba ‘anafanya kazi nzuri’ ni ‘kumtupia taulo’ la propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia Watanzania katika miaka hii miwili.
“Kwa vyovyote vile, kitendo cha Lowassa sio cha kunyamaziwa au kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.”– Lissu
lisu nataka nikuambie kuwa sio wote tuanokukubli wengine hatukukubali na tunamkubali sana raisi wetu usiseme watanzania wanaumia unaeumia ni wewe peke yako ambaye unatumika sasa basi kukutana kwa Mheimiwa lowasa na Raisi wetu mpendwa na kumpongeza sio dhambi na kuwa upinzani sio kupinga kila kitu kiukweli nawewe unatambua kuwa JPM anafanya kazi ila kwakuwa unatumika na ili upate unachokitaka ni lazima ushoboke sana, tanzania ni salama kwaninchi nyingine hakuna matukio kama hayo unayoyasema mbona yapo na tena ni makubwa tu hata huko uliko ni balaa sasa basi ningekushauri jiuguze kwanza na inaonyesha inavyoelekea unataka uwenyekiti hapo CDM maana umekuwa kitandani lakini bado unaonekana wewe ni msemaji wa chama wakati msemaji yupo. nampongeza sana Mhe Lowasa ni mwanasiasa aliyekomaa sana big up lowasa nakupongeza kwelikweli una jitambua kwenye ukweli unasema ukweli rudi nyumbani toka vichakani huko.
ReplyDeletepole lisu ufanyaji kazi wa Mhe Magufuli unakuboa eeeh mpaka unataka asipongezwe pale anapofanya vizuri imekula kwako hiyo baba unaendeleaje lakini huko uliko?
ReplyDeletenanukuu “Lakini ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na washauriane kabla ya mazungumzo hayo. Na baada ya mazungumzo, ni lazima viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote tuwe kwenye ukurasa mmoja" kwahiyo ulitaka EDO akufate akwambie sasa naenda kuonana na Mhe. Rais ili umpe kauli ya kutoa kwani yeye ana akili mpaka kauli utoe wewe kwa ushari wako yeye anaona kazi inayofanyika kwanini asiseme asubiri kushauriana na wewe na kundi lako? why mwanasheria usituburuze na edo kumpongeza magu sio kosa. mumuache mzee wawatu
ReplyDeleteTundu Lisu ni vyema ukamuomba M/Mungu akujaalie afya kamili na urudi nyumbani kwa salama na amani. Watanzania wengi wanapingana na misimamo yako ya kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali ya Magufuli ambayo kwa hakika imefanya mengi mazuri ya kupongezwa . Jitihada zako na fitna za kumkwamisha Maghufili hazitazaa Matunda hilo ufahamu. Sasa upo matibabuni nje ya nchi tunajua ni kitu amabacho wewe na washirika wako amabao ilikuwa ni ndoto yenu kupata platform yenye ukaribu zaidi na mataifa ya kigeni ili kuimwagia sumu Tanzania. Tunajua hata ile hali ya kukimbiziwa Nairobi hospital sio kwamba haukuweza kutibiwa Tanzania isipokuwa ni miongoni mwa jitihada za kuipaka matope Tanzania. Kiuhalisia hospital ya Dodoma ndio iliyookoa maisha ya Tundu Lisu na sio Nairobi hospital. Sasa serikali au Tanzania ingetaka kummaliza Tundu Lisu basi ni pale Dodoma hospital lakini wamepigana kufa kuhakikisha Tundu Lisu ana survive . Hata hatua ya kupelekwa Tundu Lisu Ubeligiji ambapo ndipo kwenye makao mkuu ya jumuiya ya Ulaya ni mikakati kabambe iliyopangwa na inayoendelea kufanywa na Chadema na wasioitakia mema kuhakikisha Tanzania inafitinishwa na jumuiya za kimataifa. Ni kampeni na jitihada maalum kuhakikisha Tanzania inatengwa na jumuiya za kimataifa zinazofanywa na akina Tundu Lisu ni harakati ambazo aliziendeleza hata kabla hajapata matatizo lakini sasa anatumia hali aliyonayo kama mtaji wa kisiasa zaidi .Mapambano ya baadhi ya wapinzani zidi ya Maghufili na serikali yake ukiyachunguza kwa makini ni mapambano zidi ya Tanzania isipige hatua kimaendeleo . Ni mapambano ya kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia kuwa ni nchi masikioni. Ni mapambano zidi ya Tanzania kuhakikisha kuwa nchi iliokisiri rushwa. Ni mapambano zidi ya Tanzania kuhakikisha watanzania wanyonge wanaendelea kutabika kuwalipia watoto wao ada za shule. Ni mapambano zidi ya Tanzania kuhakikisha rasilimali za Tanzania zikiendelea kuibiwa na kuwanufaisha wachache. Ni mapambano zidi ya Tanzania kuhakikisha miradi na mashirika ya umma ambayo yangeweza kwa kiasi kikubwa kuchangia kudhalisha ajira na ukuaji wa uchumi kama shirika la ndege la Tanzania,Tanesco,shirika la simu na mashirika mengine nchini yanaendelea kufa au kufanya kazi kwa hasara na kuwanufaisha wachache. Ni ukweli ulio wazi kabisa wanaoendelea kumpiga vita Magufuli ni watu wasiotakia mema Tanzania na watanzania. Na ningeshaa sana kumuona Edward Lowasa kuendelea kushirikiana na watu wa namna hiyo wasioitakia mema nchi yetu. Edward Lowasa ni mwananajeshi ni mtu aliekulia katika misingi ya kuilinda nchi yet kutoka kwa maadui wa ndani na nje ya nchi kwa hivyo kauli yake ya kutambua kazi nzuri inayofanywa na awamu ya tano inathibitisha yakuwa Edward Lowasa ni mzalendo wa kweli.
ReplyDelete