Kenya Yatengeneza Setilaiti Yake ya Kwanza

Kenya Yatengeneza Setilaiti Yake ya Kwanza
Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.

Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitenengeza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.

Setlaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.

Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema setilaiti hiyo ni ya umbo la mchemraba na ina ukubwa wa sentimita 10 mraba - hujulikana kama nano-setilaiti.

Setlaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mnamo mwezi Machi na kuzinduliwa rasmi kuizungukza dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.

Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa sita barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.

Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti zao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad