Kigali: Watu Wajazana Kumuona Diamond Platnumz

Nyamirambo - Kigali, Watu kutoka huku na kule walifurika siku ya Jumamosi Januari 20, 208 kumuona mubashara msanii wa kitanzania Diamond Platnumz.

Msanii huyo alikwenda sehemu inaitwa Tapis Rouge iliyoko tarafani Nyamirambo, wilayani Nyarugenge mjini Kigali, ili kuwasalimu mashabiki wake ambao walikuwa wamejitokeza kwa wingi.

Wakati wakitaraji kumuona akiwatumbuizia nyimbo zake, Diamond kwa muda wa dakika kama 20 alizokuwa sehemu hiyo hakuimba wimbo wowote bali alipita katikati ya umati wa watu akiwapungia mikono kama mfalme na baadaye kuwasambazia karanga zake za Diamond Karanga bwerere.

Diamond aliwasili mjini Kigali siku ya Ijumaa Januari 19, 2019, kwa ajili ya kuwatembelea watoto wenye ulemavu wa macho waishio tarafani Gatsata wilayani Gasabo mjini Kigali katika kituo cha Jordan Foundation, ambao aliahidi kugharamia matibabu yao kwa muda wa mwaka mmoja.

Baada ya kuwatembelea watoto hao alikutana na waandishi wa habari kwa mahojiano ambapo alipata kuzindua Diamond Karanga na Chibu Parfume na kuweka bayana mipango yake mingine ya kuanzisha Wasafi FM na Wasafi TV mwaka huu, na hata kuzindua albamu yake nyingine yenye jumla ya nyimbo zisizopungua 18, kwa mujibu wa maelezo yake.

Amesema anataka hata kufungua tawi la lebo yake ya WCB nchini Rwanda, akisema anaamini Rwanda kuna vipaji vingi lakini wasanii hawapati studio zenye uwezo mkubwa wa kuwainua kumuziki.

Amesema pia kuwa anataka kuwa na makazi Rwanda, na kesho yake alipelekwa sehemu tofauti ambazo kuna nyumba nzuri ili azikague na achague anayoona inamfaa. Kaisifia Rwanda kwa usalama na usafi na kusema ameona ana kila sababu ya kuwa na makazi Kigali.

Hizi hapa chini ni picha za jinsi watu walivyofurika Nyamirambo kumuona ambapo wengine walilazimika kusimama juu ya pikipiki zao ili waweze kumuona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad