Kigwangalla "Nawajua Vigogo Waliopanga Mauaji ya Wayne Lotter"

Kigwangalla Alitega Jeshi la Polisi Awaagiza Kuwakamata Vigogo Wanne Waliopanga Mauaji ya Wayne Lotter
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla amesema anawajua vigogo wanne waliopanga mauaji ya muhamasishaji wa utalii ‘Wayne Lotter’ mwaka jana na kulitaka jeshi la polisi liwakamate watu hao ingawaje hajawataja hadharani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma, Dkt. Kigwangalla amelitaka jeshi hilo lichukue hatua haraka za kuwakamata vigogo hao la sivyo ataenda moja kwa moja kutoa taarifa kwa Amiri jeshi Mkuu.

“Nawajua watu 4 waliopanga mauaji ya mhamasishaji wa utalii Wayne Lotter, watu hao ni vigogo na wanajulikana,“amesema Dkt. Kigwangalla.

Waziri Kigwangalla amesema ndani ya kipindi cha siku 100, Wizara yake imebaini mitandao 74 ya watu wanaojihusisha na ujangili ikiwa na washiriki 949 ambapo amedai baadhi ya washiriki hao tayari wameshafikisha Mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Kuhusu kifo cha Mwanaharakati Wayne Lotter soma zaidi kwa kubonyeza link hii “Mwili wa mwanaharakati wa tembo aliyeuawa kwa risasi kuagwa Dar“.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muheshimiwa kigwangala ni jembe kabisa Mungu amuweke. Kuja kwake katika wizara ya maliasili ni moja ya mapinduzi makubwa katika mapambano zidi ya ufisadi Tanzania katika awamu hii ya tano . Watanzania ni kasumba yetu kutovisifia au kuona thamani ya vitu vizuri vya kwetu lakini muheshimiwa Hamis kigwangala ni moja kati ya viongozi vijana wakupigiwa mfano na ni hazina ya kujivunia kwa taifa letu. Keep it up Brother. Uzalendo wake katika utendaji wake wa kazi pamoja na kiwango cha kujitolea muhanga kwa manufaa ya Taifa linamfanya kigwangala kuwa kiongozi kijana wa kipekee kabisa kitu amabacho kinatutia moyo sana watanzania yakuwa kumbe tunao vijana wanaoweza kusimamia rasilimali zetu tena kwa uadilifu wa kutisha. Ila wizara ya maliasili ni moja ya wizara zenye changamoto nzito kabisa. Wageni wamekuwa wakijinifuisha kwa hila za kujifanya wanatusaidia aidha katika masuala ya uhifadhi au uhuhishaji wa utalii lakini ukweli ni kwamba wageni hao kwa kushirikiana na wazawa wa hovyo waliopewa dhamana wamekuwa wahujumu wa uchumi wakubwa wakitumia RUSHWA kama kichocheo cha kuwadhibiti baadhi ya viongozi wa wizara kuendeleza uvunaji wa rasilimali zetu kwa njia haramu. Kwa hivyo hongera muheshimiwa raisi kwa kumuona kijana na kumuamini na hongera kwa kwake yeye mwenyewe binafsi muheshimiwa waziri kigwangala kwa kufahamu nchi yetu na watanzania na Africa wanataka nini. Hawa watu wanakuja kupora rasilimali zetu alafu watucheka kwamba nchi zetu ni za hovyo. Ni matumaini yetu yakwamba serikali inahakikisha muheshimiwa waziri anapata ulinzi wa kutosha kabisa kwani licha kazi ya kufukuwa makaburi kwenye ile wizara. Vile vile inawahalifu waliotapakaa nje ya mipaka yetu wanaoingia na kutoka na ni wizara yenye maslahi ya wahalifu wengi kuliko wizara nyingi kwa hivyo utaona wapo tayari hata kuua ili kuendeleza na kuficha uhalifu uliokwisha tendeka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad