Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Rahimu Haruni (30) ambaye anaishi mtaa wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro amefariki dunia leo wakati akianika nguo kwenye waya uliofungwa ndani ya nyumba hiyo baada ya kupigwa shoti ya umeme.
Taarifa zilizothibitishwa zinadai kuwa nyumba hiyo ambayo kijana huyo amepigwa shoto ilikuwa na tatizo la umeme ambalo lilitolewa taarifa kwenye shirika la Umeme TANESCO mkoa wa Morogoro lakini tatizo hilo lilishindwa kutatulia na TANESCO mpaka leo ambapo shoti hiyo imesababisha kifo cha kijana huyo.
Baada ya kutoa kifo cha kijana huyo kabla ya mwili wake kuondolewa ndipo mafundi wa TANESCO walipofika na kuzima umeme kwa ajili ya kuanza uchunguzi wa tatizo hilo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa kuhofia wananchi kuchukua sheria mkononi dhidi ya mafundi hao wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Kwetu sisi kila kitu siasa. Kwani Tanesco ndio waliotandika nyaya ndani ya nyumba hiyo? Pengine ukienda kwa undani zaidi nyumba hiyo imeungiwa umeme kinyemela. Kifo hakikosi sababu Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amin.
ReplyDeleteHATA KAMA SIO TANESCO WALIOTANDIKA LAKINI SIWALITAARIFIWA MAPEMA KUWA NYUMBA INA SHOTI ILI WAJE KUANGALIA NA KUTENGENEZA WANGEKUJA MAPEMA KABLA YA UMAUTI WA KIJANA MADHARA YASINGETOKEA
ReplyDelete