Kikwete na Viongozi Mbalimbali Wamfariji Mzee Kikunge Kufuatia Kifo cha Mkewe

Kikwete na Viongozi Mbalimbali Wamfariji Mzee Kikunge Kufuatia Kifo cha Mkewe
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na baadhi ya viongozi wamefika nyumbani kwa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam kumfariji baada ya kufiwa na mke wake Peras Ngombale hivi karibuni  na anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kinondoni.

Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jioni ya jana. Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam.

Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam jana.

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar.




Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuna bwana sijamuona hapa ..............yu wapi

    ReplyDelete
  2. Mimi nilimuona hata hispitali PIA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad