Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram Abubakar Shekau, ameonekana kwenye mkanda mpya wa video ikiwa ni saa 24 baada ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kutangaza hadharani kuwa kikundi hicho kimesambaratishwa.
Shekau amekiri kundi lake kuhusika katika matukio ya hivi karibuni nchini Nigeria katika maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo lile tukio la sikukuu ya Christimas katika kijiji cha Molai, mji mkuu wa Jimbo la Borno.
Shekau amejisifu kwa kusema kuwa askari wa Boko Haram wana afya njema na kwamba vikosi vya ulinzi nchini Nigeria haviwezi kufanya lolote dhidi ya wanamgambo hao.
Shekau ametoa tamko juu ya kukerwa kwake kutambuliwa kwa mji wa Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli tamko lililotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Kiongozi wa Boko Haramu Apinga Kauli ya Buhari Alioisema Katika Sikukuu ya Mwaka Mpya
0
January 03, 2018
Tags