Mchapishaji wa kitabu chenye utata kuhusiana na rais Donald Trump amesema kuwa amevikabili vikwazo kutoka kwa wanasheria wa Trump wanaojaribu kuzuia kisichapishwe.
Aidha, ametangaza wkamba amechukua hatua chapishwe mapema, leo Ijumaa.
Kitabu hicho awali kilikuwa kimetarajiwa kuchapishwa Jumanne wiki ijayo.
Kitabu hicho kijulikanacho kwa jina la Fire and Fury kilichoandikwa na Michael Wolff kutokana na upinzani mkali wa uchapishwaji wake kwa sasa kinatolewa siku nne kabla ya muda uliotarajiwa.
Mwandishi wa kitabu hicho amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba kitabu hicho kitakuwa sokoni leo.
"Kwa sasa mambo tayari, mtakisoma kesho. Asante sana Trump," amesema mwandishi huyo wa kitabu.
Fire and Fury book overHaki miliki ya pichaAMAZON
Maoni ya mambo yanayomhusu rais Trump na familia yake yaliyozungumzwa ndani ya kitabu hicho, yametolewa na aliyekuwa msaidizi wa Trump Steve Bannon, zikiwemo tuhuma familia ya Trump kukutana na watu kutoka Urusi ili kuingilia masuala ya uchaguzi wa mwaka jana