Korea Kaskazini na Kusini Zaanza Mazungumzo Kuhusu Olimpiki

Korea Kaskazini na Kusini Zaanza Mazungumzo Kuhusu Olimpiki
Korea Kaskazini na Kusini wameanza mazungumzo kuhusu mpango wa kutuma timu kwa mashinndano ya msimu wa baridi yanayofanyika mwezi ujao nchini Korea Kusini.

Korea Kaskazini ilikubali wiki iliyopita kutuma ujumbe kwenda kwa mashindano hayo, na kupunguza msuko suko kati ya majirani hao wawili kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Korea Kusini kisha ikapendekeza kufanyika mazungumzo makubwa Jumatatu kuhusi kushiriki kwa Korea Kaskazini.

Lakini Korea Kaskazini badala yake ikapendekeza kuhudhuria kwa kikosi chake cha sanaa katika mashindano hayo.

Korea Kusini imekuwa ikitaka Korea Kaskazini kushirikishwa kwenye mashindano hayo yaliyopewa jina olimpiki ya amani ikisema kuwa ni fursa ya kuboresha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Pande hizo mbili zinakutana eneo linalolindwa kati ya mataifa hayo la Panmunjom ambalo pia linafahamika kama truce village.

Wajumbe wawili kutoka kila upande walitarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo.

Wiki iliyopita wakati wa mazungumzo ya juu kati ya nchi mbili katika kipindi cha zaidi ya miaka mwilia, Korea Kaskazini ilisema kuwa itatuma wanariodha na mashabiki kwenda kwa mashindano hayo ya olimpiki ambayo yatafanyika kati ya tarehe 9 na 25 mwezi Februari mjini Pyeongchang.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad