Halima Mdee amesema hayo wakati akiongea na www.eatv.tv na kusema kuwaa Jaji Mkuu anaposema wanasiasa wasiingilie Mahakama hivyo na yeye anapaswa kusimama na kuhakikisha kuwa Mahakimu wakitenda haki na kukemea wale ambao kwa makusudi wamekuwa wakipindisha haki za watu.
"Ni zaidi ya wiki sasa Mhe. Sugu yupo ndani lakini amenyimwa dhamana kwa kosa ambalo linadhaminika kisheria na kiutaratibu kwa muhibu wa sheria zetu kama kosa linadhaminika ni wajibu wa polisi kutoa dhamana na polisi wakikushikilia ndani ya zile saa 48 wakikupeleka mahakamani ni jukumu la Mahakama kufanya hivyo sasa suala la Sugu limeenda Mahakamani ambapo huo ndiyo muhimili pekee ambao tunautegemea . Sasa unapokwenda Mahakamani sehemu pekee ambayo unaitegemea kupata haki halafu unaona hiyo haki haipatikani kwa makusudi kabisa hivyo Jaji Mkuu na yeye anapaswa kuyatambua haya na kuwakemea baadhi ya Mahakimu ambao wanafanya vitu kama hivi" alisema Mdee
Mbali na hilo Halima Mdee amedai kuwa kuna tetesi za kutaka kumfunga Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu' kama ambavyo alifungwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali
Msikilize hapa akifunguka zaidi.
Natamani hizo tetesi ziwe kweli
ReplyDeleteHalima kama unajifikiria kuwa Faiza Ally. Sugu wala hana mpango na wewe.
ReplyDeleteSugu mwenyewe amesha amua kutafuta vyombo vyake vya muziki aludie kazi yake kama nguza (baba seya)
yeye na siasa wapi na api? Au wewe na saia!!
Wacheni kutafuta kiki.