Lissu Akiri Kuwa na Deni Kubwa Nchini Kenya

Lissu Akiri Kuwa na Deni Kubwa Nchi ya Kenya
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amekiri kuwa ana deni kubwa na nchi ya Kenya kutokana na kuokoa maisha yake na kumpatia ulinzi kwa kipindi cha miezi minne aliyokuwepo nchini hapo akitibiwa.


Lissu ameyasema hayo asubuhi na mapema wakati akijiandaa kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji anakoenda kufanya matibabu zaidi kwa ajili ya viungo vya mwili ili kumuwezesha kutembea kabisa.

Akiizungumzia Kenya, Lissu amesema kwamba hataweza kusahau fadhila za nchi ya Kenya pamoja na watu wake kwani, serikali hiyo ilihakikisha inampatia ulinzi wa masaa 24 alipokuwa hospitali hapo.

"Nina deni kubwa sana na nchi ya Kenya. Wakenya wameokoa maisha yangu na kunilinda kwa wakati wote. Ninashukrani kubwa kwa serikali ya Kenya na wananchi kwani madaktari wao na wauguzi wao wamehakikisha nakuwa hivi,".amesema Lissu.

Akizungumzia kuhusu Tanzania, Lissu amewashukuru madaktari wa Dodoma kwa kuokoa maisha yake baada ya shambulio na kipekee amemshukuru Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya kwa kuwa Kiongozi mkuu wa jopo la madaktari waliookoa maisha yake na watanzania kwa maombi na michango yao.

Lissu alifikishwa Hospital ya Nairobi Usiku wa Setemba 7 baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwenye viunga vya nyumbani kwake mkoani Dodoma majira ya saa saba mchana alipokuwa ametoka bungeni.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Matibabu na ulinzi ulioupata Nairobi Hospital ni wa kulipia sio bure. Unapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kulinda uhai wako na siyo serkali ya Kenya au hospitali yao. Wamepata mamilioni ya shilingi kupitia kwako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad