Lissu Kusafirishwa Kesho Kwenda Nje ya Kenya kwa Matibabu Zaidi

Lissu  Kusafirishwa Kesho Kwenda Nje  ya Kenya kwa  Matibabu Zaidi
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amefunguka na kusema kuwa kesho Januari 6, 2018 atasafiri na kutoka nje ya Kenya kwenda kufanyiwa matibabu zaidi kufuatia shambulio la kupigwa risasi lililotokea mwaka jana.


Lissu amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa nje ya hospitali ya Nairobi na kusema kuwa amekuwepo hapo kwa takribani miezi minne akifanyiwa matibabu lakini sasa anakwenda kufanyiwa matibabu zaidi sehemu nyingine.

Mbali na hilo Tundu Lissu ameendelea kusema kuwa shambulio lake kupigwa risasi ni tukio la kisiasa ndiyo maana viongozi wa bunge wamekuwa wakishikwa na kigugumizi. Amesema Bunge limeshindwa kumhudumia na kumlipia matibabu kama ambavyo inapaswa kuwa lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa Bunge ambaye amethubutu hata kwenda kumuona.

"Leo nazungumza Bunge la Tanzania halijatoa hata shilingi moja wakati sheria ipo wazi, ndugu zangu wamewaandikia barua ya kuwaomba kupata haki ya matibabu lakini mpaka tunazungumza sasa hivi Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Bunge, Katibu wa Bunge wala hakuna kiongozi wowote wa Bunge aliyefika kuniona kwa miezi hii minne, walijua sitaweza kupona ndiyo maana hawakuwa na Plan ya kunitibu" amesema Lissu

Aidha Mbunge huyo ametoa maoni yake kuwa anaamini jaribio la yeye kutaka kuuawa mnamo Septemba 7, 2017 ni jaribio la kisiasa na amedai anaamini jeshi la polisi nchini Tanzania hawapelelezi juu ya tukio hilo.

"Maoni yangu kilichofanyika kilikuwa ni jaribu ya mauaji ya kisiasa moja kwa moja, mimi siyo mfanyabiashara, jeshi la polisi kwa maoni yangu hawapelelezi tukio hili kwa sababu sijawahi ona mtu anakuja kuniuliza, wanamtaka dereva wangu kwaajili ya kumkamata na sio kumhoji juu ya tukio hilo" amesema Tundu Lissu
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tundu lissu .... Hiyo ni Imani yako kuwa shambulio unavyo amini ni Siasa.
    Sasa utajuaje kuwa imani yako ni potofu? au Sahihi?
    au useme senti moja hukupata. Kutoka wapi?
    Wewe hasa Mwajiri wako ni Nani?

    Kama ubunge unafikiri ni Kazi .. Hapo umejidanganya.
    Ubunge ni Uwakilishi wa wananchi waliokupigia kura ili uwe sauti yao.
    Na Jinsi ulivyo sidhani kwa mtazamo wangu kuwa wewe unawawakilisha waliokupa kura.
    zaidi ya malumbano na kiki.
    Umejenga shule ngapi? Visima Vingapi.
    Umeboresha miundo mbinu mingapi?
    Umejenga Zahanati ngapi au Hospitali ngapi.
    Watanzania wanataka hayo na si vinginevyo unavyo viingilia ambavyo havina kichwa wala Miguu.
    Dua kuombea sana. Lakini hawa majambazi walitaka kukuibia muda haukua muafaka. Posho yako usiitumie
    vibaya wakazani wewe ndiyo biligeti wa TZ.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad