Lissu Kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa (The Heque)

Lissu Kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa (The Heque)
CYPRIAN Mujura ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consulotant LTD, leo kautaarifu umma kuwa kupitia wanasheria na mawakili maarufu hapa nchini wanakusudia kumfungulia mashtaka katika mahakama ya ndani na ya Kimataifa (The Heque) Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissukwa kauli zake dhidi ya serikali.



Majura amesema hayo leo Jumatatu, Jan. 15, 2017 akizungumza na wanahabari na kusema kuwa, katika Kipindi cha Focus on Africa kinachorushwa na BBC wakati akihojiwa na mwandishi Victor Kenani wiki mbili zilizopita, Tundu Lissu anadaiwa kusema Tanzania kwa sasa ni nchi hatarishi kwa siasa pamoja na pamoja na wote wanaohoji utendaji wa Serikali.



“Alisema watu wanauawa hovyo wanatupwa baharini kwenye viroba, tunataka atupe uthibitisho wa madai yake hayo ndani ya siku mbili zijazo kuanzia leo,” alisema Majura.

Majura amedai kauli hizo ni hatarishi kwa usalama wa nchi, na kwamba inaondoa amani ya nchi iliyoachwa na waasisi wa Taifa hili huku akieleza kuwa mawakili wamejipanga kumfungulia Lissu mahakama za hapa ndani ya Tanzania na wengine wanajiandaa kwenda Mahakama ya Kimataifa (The Heque).

Lissu yupo nchini Ubelgiji tangu wiki iliyopita, Jan. 6 ambako amelekwa ili kuendelea kupatiwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma mnamo Septemba 7, mwaka jana.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kumpeleka mahakamani sio issue. Lisu anajua sheria na atashinda tuu. mmeshindwa kwa risasi, mtaweza kwa mahakama?

    ReplyDelete
  2. Lisu hana cha kujua sheria wala nini ni MSALITI mkubwa ndio maana watu wamemfanyia.

    ReplyDelete
  3. Tundu Lisu hana cha kujua sheria isipokuwa ni mtu mwenye ni mbaya sana na nchi yetu. Tundu Lisu Kampeni anayoiendesha ya kuitangaza Tanzania Duniani kama Taifa hatari ni jambo la kusikitisha. Hakujawahi kutokea mtu mpuuuzi na fitna tangu Dunia iumbwe aliedhamiria kuifitinisha Tanzania na jumuiya za kimataifa kama Lisu. East to West home is the best no matter what. Afunguliwe tu mashitaka na wakati wowote akitua nchini ashitakiwe na mara hii lazima aende jela kwa sababu ni mtu mwenye kuhatarisha usalama wa taifa . Kuendesha kampeni za kulinadi nadi taifa fulani kuwa hatarishi kunahitaji uchunguzi na uthibitisho wa Umoja wa mataifa. Kauli za Tundu Lisu hazina tofauti na vitendo vya uhaini.

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo Maria Mutondi, watu wakiuawa na kutupwa maana yake serikali ndiyo imehusika, unaweza kuthibitisha hilo? kauli za Lissu si za taaluma ya sheria hata kidogo, katika sheria unapotuhumu, unapaswa kuthibitisha pasipo kuacha hata chembe ya shaka, sasa Lissu anapoituhumu serikali kwa mauaji ya watu ameweza kuthibitisha? kwa ufupi hiyo ni nature ya Lissu kusema chochote kwa watu kama Mutondi ambao mmekuja kumfahamu Lissu alipoingia CHADEMA ndiyo mnaoamini upupu anaotema, lakini kwa tunaomfahamu toka dahari hatupi taabu sana, ni MPOTOSHAJI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad