Lowassa, Njoolay Watupilia Mbali Tuhuma za Kigwabgalla ..... Sumaye Ahaidi Kumfikisha Mahakamani

Lowassa, Njoolay Watupilia Mbali Tuhuma za Kigwabgalla ..... Sumaye Ahaidi Kumfikisha Mahakamani
Familia ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Sumaye na  na Njoolay imetupilia mbali madai yaliyoelekezwa kwake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kingwangalla, jana.

Katika madai yake aliyoyatoa wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Njiro mjini hapa, Dk. Kigwangalla alidai Lowassa ni sehemu ya watu waliojipatia eneo katika eneo la mamlaka hiyo.

Msemaji wa familia ya Lowassa, Fredrick Lowassa, alitupilia mbali madai yaliyotolewa na Dk. Kigwangalla huku akisema familia yao inatambua kumiliki eneo hilo kihalali.

Akizungumzia tuhuma hizo Sumaye huku akicheka alisema, “...Nitampeleka mahakamani. Nyinyi cha kufanya andikeni hicho alichokisema vizuri ili nimpeleke mahakamani. Sina nyumba yoyote Arusha sasa kama anadhani yeye kazi yake ni kuwachafua watu acha aendelee, nampeleka mahakamani.”

Fredrick katika ujumbe wake alioutoa mara baada ya baba yake(Lowassa) kutajwa alisema, “Nimesikia taarifa za Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha.”

Alisema amesikitishwa na matamshi hayo akisema hakutarajia kutolewa na mtu mwenye wadhifa wake.

Alisema Dk Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina wataalamu wenye uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

“Nikiwa kama msemaji wa familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa,” alisema,

“Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Kigwangalla hayapo na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.”

Baadaye waziri huyo alimjibu mtoto huyo wa Lowassa akisema, “Mdogo wangu Fredrick Lowassa, tulia usiwe na hofu. Sikukurupuka kuhusu issue ya mzee wako, Ndg. Edward Lowassa, kama ana kiwanja ama la, kwenye eneo la Plot No. 4091 Njiro Arusha.

"Ukweli ni kwamba nilichokisema ni kuwa ‘tusubiri tupate majibu toka kwa mamlaka inayohusika na kutoa hati za umiliki wa ardhi kwa sababu kuna majina mengi makubwa yanasemwa... Hatuwezi kuwahukumu ama kuwataja waziwazi kwa sasa mpaka tupate nyaraka maana inawezekana wanasingiziwa.”

Njoolay, ambaye pia amewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Mwanza na Rukwa alisema, “Nimesikitishwa sana na tamko la waziri. Niliwahi kuwa kiongozi serikalini, siwezi kuwa mvamizi kwa sababu Jiji lilitangaza viwanja na sisi tukaomba na kupatiwa kama wananchi wengine.

"Kigwangalla kama alitaka kupata ukweli angekutana na sisi kwanza. Akitaka kupata ukweli aunde kamati ndogo ambayo itabaini ukweli. Kusikiliza kabla ya kutuhumu ndio utawala bora. Tunajua Serikali haifanyi kazi kwa matamko kama suala hili lipo tunasubiri barua kutoka serikalini.”

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nnachompendea lowasa ni hicho huwa ukimya wake unawapa taabu sana hawa mauchwaraz..............
    hapendi kujibishana ni mutu wa matendo kama unaona kavamia unajua pa kwenda na sheria zipo front page haisaidii

    ReplyDelete
  2. Hakuna kingine isipokuwa kama kuna watu miongoni mwa majasiri hivi sasa sio Tanzania tu bali katika ukanda wetu huu wa Africa mashariki kama sio Africa zima basi Hamis Kigwangala. Waache watakaompiga vita lakini ujasiri wake katika kuibua uozo uliofanywa na viongozi wa umma katika maeneo yake ya kazi ni ya kujitolea muhanga. Siamini wanaosema anakurupuka katika utendaji wake wa kazi bali inaonesha dhahiri wanaomlaumu ndio wenye kukurupuka. Siwezi amini Kingwala kuwa anafanya kazi bila ya kupata baraka kutoka Office kuu ya nchi na hiyo ndio inayoleta utofauti kati ya serikali ya awamu ya tano ya Magufuli na awamu nyengine. Ikiwa serikali ya Magufuli imeamua kuvunja lile jengo la Tanesco lilopo kwenye hifadhi ya barabara usitarajie kabisa kumuona akipindisha sheria katika masuala mengine yaliyotendwa ndivyo sivyo na viongozi wa Umma. Kingwala ni wa kupewa ushirikiano sio wa kubezwa. Nnaamini kabisa Kingwala anampa muheshimiwa raisi na serikali yake kile anachotaka kuona kikifanyika katika taasisi nyengine za Umma. Inashangaza sana kuona mtu aliekwisha kuwa waziri mkuu wa nchi anakurupuka kwa kusema atampleka mahakamani kigwangala. Siamini kama kweli ni kauli ya Sumaye kutaka kumpeleka mahakamni Kigwangala lakini kama ni kweli ni nia yake hiyo ni mambo ya aibu kwani Sumaye alitakiwa kufurahiwa huu mjadala badala ya kughadhibika ni kuziacha taasisi husika kufanya kazi yake na bila shaka kwa umakini na uadilifu wa serikali hii ya awamu ya tano ukweli utajulikana na kama hana kosa Sumaye hapaswi kuwa na hofu. Lakini haifai kumtisha muheshimiwa waziri kigwangala ili asite kutekeleza majukumu yake ya kazi. Ufanisi wake wa kazi muheshimiwa Kigwangala una maslahi mapana zaidi kwa taiafa na watanzania wengi hasa vizazi vijavyo kuliko maslahi ya Sumaye na Lowasa. Watanzania wengi wamekuwa na viherehere vya ushabiki wa kisiasa bila ya kuangalia ushabiki wao kama unatija kwa kile wanachokishsbikia kuliko maslahi ya Taifa yanayowagusa wao wenyewe moja kwa moja au vizazi vyao. Kuna mambo mengi ya hovyo yalifanyika na baadhi ya watendaji wasiowaaminifu serikalini katika awamu zilizopita sasa mtu mwenye akili timamu huwezi kukabidhiwa gari jipya liloibiwa vipuri alafu ukachukuwa ukaendesha tu bila kulifanyia ukaguzi halafu ukafika salama kwenye safari yako utakuwa unajidanya. Gari lazima likaguliwe ili kuhakisha safari inakuwa salama. Na kama kuna hujuma kwenye gari ilifanyika lazima gari likarabatiwe na kama kuna vipuri viliibiwa lazima ajulikane nani kaiba na wahusika lazima wajulikane ili kuepusha mkwamisho wa safari mbeleni na hicho ndicho anachokifanya muheshiwa Kigwangala na ni Matarajio yetu watanzania yakwamba kila wizara ianafanya kile anachokifanya muheshiwa Kigwangala...ikiwezekana no fear no favour katika kuutumikia Umma.Na vile vile as no favour you don't have to fear kama mtumishi wa Umma.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad