Madiwani Wengine Watatu Wajitoa Chadema na Kujiunga CCM

Madiwani Wengine wa  Chadema Wajiuzulu na Kujiunga CCM
Madiwani watatu wa Chadema, katika halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha , wametangaza kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alithibitisha leo  Januari 10 kujiuzulu kwa madiwani hao, Jacob Silas Mollel Kata ya Elang'atadapash, Elias Mepukori Mbao  Kata ya Kamwaga na  Diyoo Lomayani Laizer Kata ya Olmolog.

Mhina amesema  sababu za kujiuzulu madiwani hao wamezitoa kuwa ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi, kuinua uchumi na pia kurejesha nidhamu kazini.

"Tayari tumepokea barua zao na tumezipeleka TAMISEMI kwa ajili ya utaratibu wa kisheria ili kuwezesha kufanyika uchaguzi mdogo baada ya Tume kupata taarifa" Amesema

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido, Onesmo ole Nangole pia amethibitisha kuondoka kwa madiwani hao na kueleza chama hicho, kinafuatilia tukio hilo.

Madiwani hao kujiunga na CCM wanafanya mkoa wa Arusha pekee kuwa na jumla ya madiwani 13 wa Chadema ambao wamejiuzulu na kujiunga na CCM tangu kumalizika uchaguzi mkuu mwaka 2015.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad