Kuna mambo mawili ya kujifunza Kenya.
#Mosi; ni kuhusu Raila Odinga. Amekuwa jasiri, na mwenye msimamo thabiti wa kusimamia kile anachoamini hadi dakika ya mwisho. Ameongoza maelfu ya watu wake katika kuhitimisha safari ya "Kaanani". Kwenye kampeni aliwaambia wananchi wake atashinda, matokeo yalipotangazwa hakukubaliana nayo. Akawaaongoza watu wake kuyakataa. Na leo ameungana nao kujiapisha.
Bila kujali vitisho kutoka vyombo vya dola, bila kujali kuwa anaweza kushtakiwa kwa "uhaini" lakini amejivika ujasiri. Hili ni funzo kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa barani Afrika. Sio unawaambia watu "pigeni kura matokeo niachieni mimi" lakini siku ya matokeo unajifungia ndani, halafu baada ya miaka miwili unaenda kupongeza juhudi. If people grant their trust on u, please learn to fight your battle to the last.
#Pili; ni kuhusu Rais Uhuru Kenyatta. Huyu ni kielelezo cha kiongozi wa mfano bora kabisa wa demokrasia duniani. Ameonesha "political maturity" ya hali ya juu sana. Kama ni soka huyu ndiye "man of the match" kwa leo.
Mwanzoni vyombo vya usalama vilitishia kusambaratisha kusanyiko hilo la Raila. Ni wazi wangefanya hivyo yangetokea machafuko makubwa sana nchini humo na huenda sasa hivi tungekua tunasambaza picha za majeruhi na marehemu na hashtag isemayo "Pray 4Kenya"
Lakini Uhuru ametumia hekima ambayo viongozi wengi wa Afrika wamekosa. Ameamua kuwaacha wafuasi wa Raila waridhishe mioyo yao. Wakati wafuasi wa Raila wanafika uwanjani tayari Askari walikua wametanda viwanjani hapo na silaha nzito. Uhuru alijua kwamba pamoja na kuzuia askari wasishambulie raia, lakini wafuasi hao wangeweza kuwachokoza askari na hatimaye kuzusha taharuki. Kwahiyo akaamua kuwaondoa askari wote uwanjani.
Hii ni busara ya hali ya juu sana. Sio viongozi wengine wamejaa mihemko wakiona tu watu wamekusanyika na tishert za "Pray4Somebody" wanaagiza wapigwe. Huku ni kuyatumia vibaya majeshi. Ukiona hata katuni unakasirika. Ebo.!! Kiongozi ni lazima ujifunze kuzuia mihemko yako. Mtu amepigwa risasi, watu wamekusanyika kwa amani ili wamuombee, unaagiza Polisi kuwasambaratisha kwa mabomu. Kama kusanyiko la kumuombea tu mtu linakupa mihemko, vp ukisikia kuna kiongozi anataka kujiapisha kama Raila?
Kuna wakati viongozi husababisha maafa bila sababu yoyote kwa kuvitumia vibaya vyombo vya ulinzi na usalama. Ni muhimu viongozi wa Afrika wajifunze busara ya Uhuru kwamba si lazima matumizi ya nguvu kila mahali. Uhuru anajua hamna Ikulu mbili, hakuna cabinet mbili, hakuna mabunge mawili. Anajua Raila amejiapisha kujifurahisha tu na kukata kiu ya wafuasi wake. Lakini at last atarudi nyumbani akale "gideri" na mke wake. Sasa kwanini ajihangaishe kupiga mabomu na kuua watu bure? This is the true meaning of democracy.
Salaam kwa Faru John.!
Malisa GJ.