Klabu ya Manchester City inakaribia kumsajili beki wa Athletic Bilbao inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispania La Liga, Aymeric Laporte kwa dau la paundi milioni 57.
Meneja wa Man City, Pep Guardiola amevutiwa na kipaji alichonacho beki huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 na hivyo yupo tayari kukabiliana na kipengele cha kumsajili mchezaji huyo.
Dili la kumnasa beki huyo wakati, Laporte linatarajiwa kukamilika kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Jumatano.
Endapo City itafanikiwa kukamilisha usajili huo wa paundi milioni 57 itakuwa imevunja rekodi yake baada ya mara ya mwisho kufanya usajili mkubwa ilikuwa ni paundi milioni 55 ilipomnasa Kevin de Bruyne mwaka 2015.
Kiungo huyo wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne ambaye amejiunga akitokea Bundesliga katika klabu ya Wolfsburg hivi karibuni ameongeza mkataba wake na City utakao mfanya aendelee kusalia katika timu hiyo mpaka mwaka 2023.