Man Fongo Atokwa na Povu

 Man Fongo  Atokwa na Povu
Msanii wa miondoko ya singeli Man Fongo amewaomba wasanii wenzake kama kuna yeyote yule anahisi amemuibia kazi yake ya sanaa kwa namna moja ama nyingine basi asisite kwenda kumshtaki Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ili waweze kuhakiki haki miliki.

Man Fongo amebainisha hayo baada ya kusakamwa takribani wiki moja sasa kwa kudaiwa kutumia kazi ya wasanii wenzake bila ya makubaliano ya aina yoyote waliyowekeana.

"Ni kweli nimepigiwa simu na watoto wa Baraka Mwishee wakitaka kufuatilia hati miliki ya ule muziki. Kwa hiyo hata kama kuna mtu mwingine anaona mimi nimemuibia muziki wake asiogope kufuatilia hati miliki kwa sababu huu muziki wetu tunausajili BASATA. So ukiwa unaongea ongea mimi najua ni 'blah blah' tu hizo wanaotafuta kiki kutoka kupitia mgongo wangu", alisema Man Fongo pindi alipohojiwa katika kipindi cha eNewz kutoka EATV.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad