“Kushinda dhidi ya Azam si kitu kidogo, ni timu nzuri ambayo naikubali kwa Tanzania lakini nashukuru tumeweza kupata ushindi dhidi yao”-amesema Cannavaro ambaye ni mchezazi wa muda mrefu zaidi kwa sasa kwenye kikosi cha Yanga.
Licha ya kutocheza katika mchezo huo, Cannavaro anaamini matunda ya ushindi huo ni umoja uliopo kati ya wachezaji wanaocheza na wale wa nje ya uwanja.
“Nimefurahi kwa sababu yanga ni kama familia tunashukuru tumeweza kupata ushindi na watu wote wanaocheza na wasiocheza tumekuwa kitu kimoja na kuweza kupata pointi tatu ugenini.”
Mkongwe huyo amesema tayari kama wachezaji wameshakubalina kushinda kila mechi inayokuja mbelke yao: “Tumekubaliana kwamba ili tuweze kutetea ubingwa ni lazima tushinde mechi.
Licha ya ushindi dhidi ya azam kuifanya yanga ipunguze pengo la pointi, cannavaro bado anawaheshimu wapinzani wao wanaoongoza ligi kwa sasa.
“Bado ligi ni ngumu na tumeachwa na Simba, mpira wa kitanzania haujapishana sana ikiwa tutachanga karata zetu vizuri tunaweza kutetea ubingwa wetu vizuri.