Mbali na ubalozi huo, Umoja wa Ulaya (AU) nao umesema unategemea kuona maendeleo mazuri kutokana na uchunguzi wa tukio hilo unaoendelea.
Familia ya Lissu na chama chake cha Chadema vimekuwa vikisisitiza haja ya uchunguzi wa shambulio dhidi ya Lissu lililofanywa na watu wasiojulikana mjini Dodoma, ufanywe na taasisi huru na mwishoni mwa wiki mwanasheria huyo wa kujitegemea aliomba jumuiya ya kimataifa iingilie kati.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limekuwa likisema kuwa bado lina uwezo wa kuchunguza tukio hilo.
Pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alisema uchunguzi ulikamata magari zaidi ya kumi 10 yanayofanana na lililotajwa kuhusika katika tukio hilo, lakini hakuna mtu aliyekamatwa.
Baadaye Oktoba 8, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro alisema mjadala wa tukio hilo umefungwa.
Kwa sasa Lissu, aliyekuwa akitibiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ameruhusiwa kutoka na amehamishiwa Ubelgiji kwa matibabu ya awamu ya pili yakayohusisha mazoezi baada ya mifupa yake kuharibiwa na risasi katika shambulio hilo la Septemba 7.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema jana kuwa chombo hicho hakizungumzii suala la Lissu.
Akijibu swali la gazeti lililomtaka kutoa maoni yake kuhusu kutokubaliwa kwa wachunguzi wa kimataifa kusaidia upelelezi dhidi ya shambulizi la Lissu, ofisa ubalozi wa Marekani nchini alisema kwa njia ya barua pepe kuwa itakuwa tayari kutoa ushirikiano wake ikiwa itaombwa na Serikali ya Tanzania.
“Wakati Serikali ya Marekani huko nyuma imekuwa ikitoa ushirikiano katika baadhi ya uchunguzi wa kimataifa, kufikiria uwezekano wa kushiriki, utahitaji kwanza ombi la msaada kutoka Serikali ya Tanzania,” inasema barua pepe kutoka ubalozi wa Marekani.
Barua hiyo pepe inataka mtoaji taarifa hiyo anukuliwe kama ofisa ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.
Lissu alishambuliwa wakati akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma, akiwa ndani ya gari lake.
Mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kuwa nyumba hiyo ni moja ya zile za viongozi zilizopo eneo hilo ambazo zinalindwa wakati wote na kwamba eneo la kuingilia kwenye nyumba hizo lina geti ambalo hukaa askari wakati wote, lakini siku hiyo hawakuwepo.
Kama Marekani wataombwa kushiriki uchunguzi huo, haitakuwa mara ya kwanza kuja nchini. Mwaka 2013 Shirika la Uchunguzi la Marekani (FBI) lilichunguza mauaji ya aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mpendae, Padri Evarist Mushi aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Hata hivyo, mtuhumiwa aliyebainishwa na FBI, Mussa Omar Makame alikuja kuachiwa na Jeshi la Polisi baada ya ushahidi kutotosha kumtia hatiani.
Mbali na kauli hiyo ya ubalozi huo, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Balozi Roeland van de Geer ameliambia gazeti hili kwa njia ya barua pepe kuwa jumuiya hiyo imekuwa ikifanya majadiliano na Serikali kuhusu masuala ya haki za binadamu, siasa na uchumi yanayoibuliwa na kwamba unaamini uchunguzi wa shambulio la Lissu utapiga hatua.
“Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake wana mazungumzo ya mara kwa mara yakiwemo ya kisiasa yaliyowekewa utaratibu rasmi, masuala yanayohusu haki za binadamu pamoja na siasa na kiuchumi kwa pande zote, Tanzania na Ulaya huibuliwa na kujadiliwa,” inasema baruapepe ya Balozi Geer.
“EU na wanachama wake na Tanzania wataendelea na mazungumzo haya ikiwa ni pamoja na matukio ya kisiasa ya hivi karibuni. EU inaamini kuwa kutakuwa na maendeleo katika uchunguzi wa jaribio la maisha ya Lissu.”
Hata hivyo, Wakili maarufu nchini, Dk Onesmo Kyauke alisema suala la kuita vyombo vya kimataifa kuchunguza ni gumu kwa sababu linaingilia mamlaka ya ndani ya nchi.
“Kila nchi ina vyombo vyake vya usalama vinavyoshughulikia uhalifu wa ndani. Nchi inaweza kuomba msaada wa kimataifa kama kuna makosa yaliyovuka mipaka kama ugaidi au kutakatisha fedha, lakini makosa ya ndani inakuwa vigumu, kwa sababu lazima waseme wameshindwa,” alisema Dk Kyauke.
Alisema bado ana imani ya vyombo vya ndani vya usalama, hata kama vimekaa kimya.
Aliongeza kuwa sheria zinaruhusu watu kufanya uchunguzi wao binafsi, lakini pia zinaruhusu mwendesha mashtaka wa Serikali kuuchukua uchunguzi huo kwa manufaa ya Serikali.
“Zipo sheria zinazoruhusu watu kufanya uchunguzi wao binafsi, lakini pia sheria hizo hizo zinampa mamlaka DPP kuchukua suala hilo kwa manufaa ya Serikali.”
Alipoulizwa maoni yake kuhusu suala hilo, Profesa wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa, Gaudence Mpangala alisema shambulio la Lissu limeshachafua taswira ya Tanzania kimataifa.
“Hili suala lina impact (athari) kubwa kimataifa, siyo la kuchukulia kijuujuu,” alisema.
Profesa Mpangala alipendekeza kuwepo mjadala kujadili demokrasia na uhuru wa maoni.
Alisema ni muhimu kujadili suala hilo kwa kuwa hata wakati wa mfumo wa chama kimoja, muasisi wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alikubali kukosoa Serikali.
Chanzo: Mwananchi
kim jong amewashinda mje tz vichekesho
ReplyDeleteWatanzania wengi ni watu tunaoona fahari kujidhalilisha hasa kwa wazungu. Wazungu kwa hakika kabisa wanajua sisi ni watumwa wa nafsi zetu linapokuja suala la kujipendekeza juu yao. Katika nchi zao kuna matukio ya akina Lisu mengi sana tu tena mengine yametokea hata kabla Tundu Lisu hajazaliwa na mpaka hii leo hayajapatiwa ufumbuzi na kesi nyengine mafaili yao yameshafungwa. Yule Mbeligiji, Mjerumani,Muengereza, Mspania, Mreno We acha tu achana na hao watu tema mate chini. Sisi waafrica kama tungekuwa watu wa kujitambua basi hata ingekuwa vipi hata ingetokezea akina Tundu Lisu kumi kujeruhiwa basi isingekuwa busara kukimbilia au kutamani kwenda kuwaita wale watu kuingilia mambo yetu ya ndani. . Usione hivi sasa wanajitia waumgwana mambo yao wanayafanya kisayansi zaidi kufunika kombe ili mwanaharamu apite lakaini hata hivyo bado hawana msalie mtume hata kidogo kwa mtu amabe atakinzana na maslahi yao ya taifa au mtu au taifa watamshughulikia tu. Huyo Mmarekani kwenda kumlalamikia suala la Tundu Lisu hakuna chengine chochote isipokuwa ni kutafuta kiki za kisiasa.
ReplyDeletetanzania ina utawala wake na atuwezi kukubali kusujudia wazungu sisi wenyewe tunaweza hatufikirii wala hatotofikiria kuwa na akili za kubebwa kiasi hiki swala ni la klwetu tutalifatilia wenyewe uwezo upo hivyo ilo wazo la kusema wamerekani waruhusiwe sahau tena halipo kama wanataka waende kwanza kwa kim korea kaskazini. acheni kutafuta kiki za kipuuzi kwanza marekani hakuna matukio kama ya kina lisu nani amekwenda kuchunguza fikiri kabla ya kutamka.
ReplyDeleteKwanza hawapendi maendeleo ya bara hili, na wanapenda kumuona mtu mweusi ni wa chini siku zote mpka wanafikia hatua ya kutuita IQ ndogo mara sub human. Hawana Lolote, tena wanapenda kuona Africa ikiwa na migongano vita corruption, wanajua ndio wanazidi tajirika corruption za Africa na kuwaita hata viongozi hao hao corrupt stupid leders wameshindwa kujiongoza Africa, Sasa wakisha ona kuna kiongozi imara Africa hawapendi, wanatafuta kila sababu ya kuwangusha watupishe sisi kuleeeee washughulike na ya kwao, hawana hata collaborate ya maendeleo ya bara hili Bali wanapenda na kufuraia shali za bara hili, ili wapate kuiba vizuri msuuuu
ReplyDeleteHasa hawa wanaojita Wamarekan, hawana huruma hataa. Si manigger sisi, Sasa Nini? Wanachotaka kuangaika na manigger na watu wa IQ ndogo akili ndogo, mara sub human Yaani yote hayo majina ni wao wamarekani Lol. Mtu mwenyewe mweusi wa marekani hawamuoni kama mmarekani kutwa kuwambia warudi Africa kwao wakati alipelekwa utumwa huko, ndio itakuwa sisi wa huku Africa asilia
ReplyDelete