Maskini Kingunge Apokea Kwa Masikitiko Taarifa za Kifo cha Mkewe


Maskini Kingunge Apokea Kwa Masikitiko Taarifa za Msiba wa Mkewe
Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru leo Jumamosi amepewa taarifa za kifo cha mke wake Pares Mwiru ambazo imeelezwa kuwa amezipokea kwa mshtuko mkubwa.

Kingunge aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Kijitonyama, alifanyiwa upasuaji Januari 4 mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 6, mtoto wa mwanasiasa huyo Kinje Mwiru amesema wamempa taarifa baba yao saa tano asubuhi leo.

“Tumemfahamisha nusu saa iliyopita, ilikuwa ni vigumu sana wakati tunamfikishia taarifa hizo na amezipokea kwa ugumu sana. Haikuwa rahisi kwa yeye kupokea taarifa wakati tunamweleza,” amesema.

Kinje amesema kwa sasa wamemuacha apumzike ili aweze kuwapatia mwongozo nini kifanyike baada ya kifo cha mke wake.

Pares alifariki Januari 4 saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa, tangu alipofikishwa Muhimbili Oktoba 3, mwaka jana.

Akizungumza na Mwananchi leo, Ofisa Uhusiano wa MNH John Stephen amesema kwa sasa afya yake imeimarika.

Soma: Rais Magufuli afika Muhimbili kumwona Kingunge

 "Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad