Maskini!... Radio Hali Yake Bado Mbaya Baada ya Kupoteza Fahamu Kutokana na Kipigo

Maskini Radio Hali Yake Bado Mbaya Baada ya Kupoteza Fahamu Kutokana na Kipigo
Msanii wa muziki wa nchini Uganda Moses Nakintije Ssekibogo maarufu kama Radio, bado anaendelea kupigania uhai wake kwenye hopsitali ambayo amelazwa nchini humo, baada ya kupoteza fahamu kutokana na kipigo.

Taarifa kutoka kwa uongozi wake umesema Radio bado hajitambui ingawa ameanza kutingisha vidole, na hadi sasa ameendelea kuwa kwenye comma akipigania uhai wake

"Sasa hivi anaweza kutingisha vidole, anapigana sana sasa hivi ingawa madaktari hawataki atoke kwenye comma sasa kutokana na reaction ya mwili, inaweza ikaleta madhara kwenye dawa anazotumia, hivyo anahitajika kupumzika", umesema uongozi huo.

Radio alipata comma baada ya kupigwa na watu ambao hawajajulikana mpaka sasa kwenye ugomvi, alipokuwa akitoka kwenye hoteli moja mjini Kampala akiwa kwenye parking ya gari, na kupoteza fahamu.

Wasanii mbali mbali wa nchini humo wamekuwa wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii, kumuombea aweze kupona haraka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad