Maulid Mtulia Achukuwa Form Tayari Kugombea Ubunge Kinondoni


Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), kisha kuhamia CCM, Maulid Mtulia leo Januari 17, 2018 amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama tawala.

Amechukua fomu hizo hizo za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika ofisi za manispaa yaKinondoni.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku nane zilizopita Mtulia kutii agizo la chama hicho lililomtaka kuripoti ofisi ya CCM mkoa kwa ajili ya kuchukua maelekezo ya uchaguzi.

Hivi karibuni CCM kilitangaza kuwarudisha kugombea majimbo yao waliokuwa wabunge, Mtulia wa Kinondoni na Dk Godwin Mollel (Siha-Chadema) ambao wamejiunga na chama hicho tawala.

Mtulia alipoulizwa nini ambacho anawaeleza wananchi wa Kinondoni, amesema siku ikifika atazungumza mengi.

Uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo ya Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika Februari 17 baada ya NEC, kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge Job Ndugai ikieleza majimbo hayo yapo wazi.


Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sina chama na wala sihitaji kuwa na chama manake nikiwa nisiwe haniongezee wala hanipunguzii, ila kwa hiki ninachokiona naomba wananchi wa kinondoni msikubali ujinga huu ujirudie ni bora kukaa kimya km mimi, kuliko kumchangua mtu kesho anajivua keshokutwa anagombea tena, halafu bado mnaamka asubuhi kwenda kupanga mistari kumchagua yule yule tena kweli? HAPANA

    ReplyDelete
  2. Huyu hastahili kuchaguliwa tena. Hajui kazi yake na madhara makubwa aliyoyasababisha. Alishakuwa kiongozi hapo kwa kuwatumikia watu hapo. Sasa atawatumikiaje tena watu hao hao tofauti ni nini. Ukisikia wajinga wasiojijua na wasiozijua kazi na umuhimu wa kazi zao. Kwa sababu binafsi amaliingizia taifa hasara kubwa sana kwa kujitakia umaarufu tu kupitia CCM na kupendwa na kumridhisha mtu mmoja , Raisi tu. Na watu kama hawa ni hatari nchini sababu anamuunga mtu na si Taifa. Sijui angependa ateuliwe waziri kama wengine walivyoteuliwa, Ni vibaraka wakuu wasio na elimu na kazi zao ni kupotosha umma kwa maslahi binafi.
    Msimpe kura huyu kibogoyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad