Mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe amedai amesikitishwa na namna inavyoendeshwa kesi ya Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga iliyoahirishwa leo.
Freeman Mbowe ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari hii leo katika viunga vya Mahakama ya mkoani Mbeya mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuzitaka mamlaka husika zinazosimamia sheria nchini kujiangalia vizuri katika utendaji kazi wake.
"Tumesikitishwa kwa namba suala hili jinsi lilivyo shughulikiwa, sipendi kuingilia uhuru wa Mahakama, mienendo ya kimahakama lakini mimi kama raia na kiongozi nafikili vyombo vinavyostahili kutoa haki kwa wananchi vinawajibu wa kujiangalia vizuri.
"Mahakimu, Majaji, Mawakili wa Serikali pamoja na Askari wenyewe hawa wote ni binadamu haina maana kwamba wao hawawezi kufanya makosa wao ni binadamu kama walivyo wengine", alisema Mbowe.
Kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga imehairishwa leo na kutajwa kusikilizwa Februari mbili baada ya Mawakili watatu kujitoa kuwasimamia katika kesi hiyo.
Kwani ishawahi kutokea Mbowe na Chadema kokosa jambo la kulalamika linapokuja suala la kusahihishwa pale wanapokosea?
ReplyDeletewEWE mTOWE UMEKUWA kIONGOZI...???
ReplyDeleteJamani ... jama.. Toka Lini!!!...?
Kiongozi wa Nchi Gani au Wilaya Gani..!!??
Mbona mnatuficha kisili sili... mnapata uongozi na sisi Hatujuiii.
Vibaya Hivyo Mtowe.
Lazima tufufanyie Pati ya Hongela mwanangu kuwa Kiongozi.
Kiongozi Hasa ....!!! Au unatania...?