Mbunge Ataka Chips Kuanza Kusafirishwa

Mbunge Ataka Chips Kuanza Kusafirishwa
Mbunge wa Njombe Mjini, amewataka wajasiriamali wadogo mkoani Njombe kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo na kuanza kusafirisha viazi ambavyo tayari vimecharagwa chips ili kuepuka kulaliwa na wafanyabiashara wanaolazimisha kufunga lumbesa za viazi.


Edward Mwalongo amesema hayo akiwa anaongea na baadhi ya wajasiriamali mkoani humo ambao wameanzisha kiwanda kidogo cha kumenya viazi na kucharanga chips na kudai kuwa wana Njombe wanapaswa kuvitumia viazi kama malighafi yao ambayo inaweza kuwaletea viwanda vingi vidogo vidogo.

"Viazi ni sehemu ya malighafi ambavyo tungeweza kuvitumia kama hivi na huo ndiyo mwanzo tuitumie malighafi ya viazi ili kusudi tuanzishe viwanda vidogo vidogo vingi kadri inavyowezekana, kwa sababu kila kiazi kinachotoka Njombe kikisafirishwa hakipelekwi kwa ajili ya mbegu bali kinakwenda kuliwa na kama kinakwenda kuliwa kinaliwa kama chips au kinakwenda kumenywa lakini sehemu kubwa inajulikana vinakwenda kuliwa kama chips sasa tufike mahala wana Njombe badala ya kulalamika na Lumbesa tuanze kusafirisha chips zilizomenywa kwa kuweka kwenye ubaridi na ziwafikie walaji" alisisitiza

Mbunge huyo wa Njombe Mjini aliwakabidhi mashine ya kukatia viazi wanawake wajasiriamali ambao wameunda kikundi chao na kuanza kufanya kazi hiyo ya kukata chips na kuziuza kwenye mahoteli, migahawa na wapishi wa chips mkoani humo.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad