MC Pilipili Aipongeza Serkali kwa Kuwabana Wanoatupia Picha za UCHI Mitandaoni .....Aitaka Pia Imuhoji Idris na Kim Sasha

Baada ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumuita msanii wa Bongo Fleva Gigy Money na Mwanamitindo Sanchoka kwa mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zinaonekana zipo kinyume na maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa, Hatimaye Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, MC Pilipili ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kuishauri iendelee kuwasaka wengine wanaofanya hivyo.

MC Pilipili amesema amepokea taarifa hizo kwa mikono miwili ingawaje amesema kuna watu wengi mitandaoni wanafanya makosa kama hayo ya kuvaa nguo fupi au kuonesha maungo yao kwenye mitandao.

“Hiyo hatua mimi nimeipenda kwanza imeturudisha kwenye Maadili..Unajua hapa Bongo mtu anaweza akawa maarufu kwa kuposti maumbo yake tuu mtandaoni hii ni kinyume cha maadili,“amesema MC Pilipili na kuwataja watu wengine wanaokaa uchi mitandaoni

“Nilipatwa na maswali juzi Sancho ameitwa, Gigy Money kaitwa lakini pia kuna msanii mwingine alikuwa maarufu kwa kuposti picha kama hizo amejichora mitatuu anaitwa Agness, mwingine anaitwa Kim Sasha lakini wakati huo namuona Idris naye amevaa chupi hivi ile haihamasishi au naye aitwe?“amesema MC Pilipili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad