Meli Nyingine Yenye Bendera ya Tanzania Yakamatwa Ugiriki Ikiwa na Vifaa vya Silaha


Serikali ya Ugiriki imeikamata meli yenye usajili wa Tanzania, ikielekea nchini Libya huku imebebea vifaa vya kutengeneza silaha.
-
Umoja wa Mataifa na Ulaya uliweka vikwazo vinavyozuia kuuza au kupeleka silaha Libya tangu mwaka 2011
-
Je, Nini chanzo cha Meli za mataifa mengine kutumia bendera ya Tanzania?
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani haya mambo ya bendera yetu ya Taifa kuhusishwa na uharamia na uhalifu kunakohusiana na kukamatwa kwa meli kadhaa zilizobeba bendera ya Tanzania duniani sio jambo la kulichekea tena. Kuna mambo kadhaa wa kadhaa hapa. kwanza kabisa inawezekana kabisa kutokana na vitendo vya ufisadi vilivyokwisha kutuathiri nchini kwa baadhi ya watanzania hasa wale watanzania waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi mbali mbali nchini kutokuwa waaminifu kumepelekea kuuzwa bendera yetu kwa kikundi au magenge ya uhalifu duniani hasa katika kusajiliwa hizi meli chini ya bendera ya Tanzania kinyemela unaofanywa na baadhi ya maofisa wa usajili wa meli hapa nchini. Tunajua baadhi ya watumishi wasiowaaminifu wameifanya nchi hii kuwa miliki ya makundi ya wahalifu duniani kwa muda mrefu sasa kwa kuchukua rushwa kwa maslahi yao binafsi, tunataka hii tabia ikomeswhe na wahusika wachukuliwe hatua. Tunajua serikali ya Magufuli na ile ya Muungano inao uwezo wa kukomesha vitendo hivi kwa hivyo tunatarajia kuona uchunguzi wa haraka na kina kuliko hata ule wa makinikia ukilishughulikia suala hili. Ni hatari kwa mtanzania wa kawaida asiekuwa na hatia kuonekana muhalifu katika jamii za kimataifa kwa kosa linafanywa na watu wa mataifa mengine. Bendera yetu baada ya kuitanagaza nchi kwa mambo mazuri sasa inaitangaza Tanzania katika masuala ya kigaidi pengine ni chama njama za makusudi zinazofanywa na maadui wetu wa nchi kutuchafuwa duniani. Ni suala la kuchukuliwa serious kwa kila mtanzania kwa usalama wetu binafsi na Taifa kwa ujumla.

    ReplyDelete
  2. Swadakta mdau.
    Benders yetu Ni alama yetu na utambulisho wetu kimataifa
    Suala hili tulipe uzito stahiki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad