Ni story ya kuamkia January 31 mwaka 2011. Eneo ni makaburi ya Mwananyamala hospital, njia ya kuelekea kwa Kopa (Hadija) Msisiri 'B'
Ilikuwa ni mshtuko mkubwa baada ya asubuhi ile nje ya nyumba ya mzee Mwarabu mkabala na makaburi hayo kwenye shina la miwa ulipoonekana mkono wa kichanga. Tahadhari ilichukuliwa na haraka ripoti ikafika polisi.
Taratibu za kipolisi na kutafuta usafiri zilizochukua takriban dakika 45, walikuta tayari kaburi limewekewa mauchafu na kupigwa kibiriti. Mshangao ukatamalaki. Kuuliza ni nani kafanya vile mashuhuda wakasema ni James Ngomero.
James Ngomero ni nani?
Haijulikani hasa asili yake lakini inasemekana ni mwenyeji ama alitokea Lushoto Tanga. Alianza kujulikana wakati anafanya kazi kwenye duka la mama mmoja, kazi ya kubeba mizigo, ambapo hata hivyo aliharibu na kufukuzwa kazi.
James alikuwa kapanga chumba kimoja cha giza hapa mkabala na makaburi. Sasa baada ya kufukuzwa kazi akawa hana ishu tena zaidi ya kushinda pale makaburini na kutafuta ishu yoyote ya kumuingizia kipato. Taratibu akaanza kuzoeana na wafanyakazi wa manispaa upande wa makaburi waliokuwa wanakuja kuzika maiti zisizo na ndugu.
Sasa kwakuwa James ni kijana barobaro mwenye nguvu akawa anapewa tenda ya kuchimba makaburi na wale wafanyakazi wa manispaa
Kadiri siku zilivyosonga ndio walizidi kujenga mazoea na hatimaye kuaminiana kiasi kwamba kuna wakati alitumwa mpaka mochwari na kusaini na kuchukua maiti na kwenda kuzizika mwenyewe.
Fursa hii adhimu hakuilazia damu. Akajenga mazoea na watu wa mochwari pia. Sasa ikawa wale wafanyakazi wa manispaa wakitoka kazini James anaenda mochwari kutega mingo na ikipatikana maiti anaenda kuzika kimya kimya bila kuwajulisha mabosi zake.
Jamaa walipokuja kugundua hilo walimtimua kibarua na kumpiga stop kukanyaga makaburini. Hali ikawa ngumu kwake. Ikabidi atafute kazi nyingine. Mungu si athumani akapata kazi ya ulinzi wa usiku. Lakini sasa tayari alikuwa ameshajenga mtandao na watu wa mochwari. Na kwa kawaida vichanga vingi vilivyokufa havikuwa na process huku baadhi ya ndugu kwa mila taratibu zao hawakurusiwa kubeba maiti au waliona usumbufu hivyo kumalizana tu na watu wa mochwari.
James kazi inambana usiku kwahiyo alichokuwa anafanya akitoka kazini anaenda mochwari anachukua mzigo kwenye rambo anaenda kuhifadhi nyumbani kwake mpaka jamaa wa makaburini waondoke kisha fasta ataenda kufukukia na kuwahi kibaruani.
Mbinu hii ikastukiwa na wale jamaa wa makaburini hivyo wakaweka mashushushu. James hili akalinasa sasa afanyeje akawa ana uwezo wa kukaa na maiti ndani ya chumba chake mpaka siku tatu na siku akipata mwanya ataibuka usiku wa manane na kwenda kuzika.
Kuna nyakati alibanwa sana mpaka maiti ikaanza au zikaanza kuharibika ndani ya chumba.. Hivyo alichokuwa anafanya ni kwenda kuzidumbukiza chooni... Hali hii ilipelekea choo kunuka na kutoa harufu kali kwa siku kadha bila wapangaji kuelewa hali hiyo inasababishwa na nini.
Kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa na vifo vingi sana vya vichanga pale Mwananyamala hospital na kutozingatia taratibu za kazi na kutaka kipato cha haramu. Wafanyakazi wa mochwari wakawa wanamtumia James kama mtu wao wa kuzika. Ilifika mahali sasa James ana baiskeli na anafunga maiti mpaka tatu bila kujulikana na kwenda kuzisunda chumbani kwake. Yani akawa ana mochwari yake ndogo nyumbani.
Hali ya chumba chake cha kuishi
Ndani kulikuwa na kigodoro kimoja cha wagonjwa alichokipata Mwananyamala hospital kwa njia ajuazo. Mashuka yake pia yalikuwa ya hospital tena yenye nembo ya MSD (angalia picha) hiki chumba kilitumika kama mochwari pia. Kuna siku jamaa yake alikuja na demu kufanya yake, sasa baada ya kumaliza anatafuta cha kujifutia akaona shuka imeviringwa pembeni mwa chumba, kulifunua alikutana na mwili wa kichanga, alifunika fasta na kunyuti. Mungu bariki chumba kilikuwa na giza hivyo demu hakustuka.
Siku ya Tukio
Wiki ile ya January 31 mzigo ulikuwa wa kutosha, tayari ndani alikuwa na maiti za vichanga 11 na nyingine zilikuwa zimeshaanza kuharibika hivyo ili kuokoa jahazi lisizame na aweze kuingiza mzigo mpya ilibidi maiti zile zizikwe usiku ule ule.
Tukiwa na James kwenye pub moja Sinza njia ya kuelekea Wanyama hotel tulilewa mpaka saa mbili usiku. Baada ya hapo tukahamia Royal bar Mwananyamala tuliendelea pale mpaka saa tano usiku hivi na kumuacha James Ngomero pale. Kumbe siku hiyo alikuwa na hiyo mishe kwa hiyo ilipofika usiku wa manane akaenda kuzizika zile maiti nje ya nyumba ya mzee Mwarabu karibu na shina la miwa na pengine kusahau mkono uliokuja kuonekana ama la kuna mtu alikuja kufukua.
Jinsi niivyomfahamu James
Nimeishi Mwananyamala karibu kabisa na hospital kwa miaka kumi. Ni katika kipindi hicho nilipata misiba ambayo ndio ilisababisha kumfahamu James. Lakini misiba yangu ilikuwa official na alitusaidia kwenye kuchimba makaburi.
James alikuwa msiri wa maisha yake na ni ngumu sana kujua vyanzo vyake vya mapato. Alikuwa mlevi kupindukia na inasemekana pia alijihusisha na biashara ya viungo vya binadamu. Pamoja na yote hayo hakuwa hata na kitanda. Baada ya habari ya maiti 11 za vichanga James alikimbilia kusikojulikana huku wafanyakazi wa mochwari na walinzi wakifukuzwa kazi
Source:JF
Mfahamu James Ngomero: Mmtuhumiwa wa zile Maiti 11 za watoto Vichanga Hospitali ya Mwananyamala
0
January 19, 2018
Tags