Mfungwa Aliyedaiwa Kufa Afufuka Akiwa Chumba cha Kuhifadhia Maiti

Mfungwa Aliyedaiwa Kufa Azinduka Akiwa Chumba cha Kuhifadhia Maiti
Mfungwa mmoja kaskazini mwa Uhispania alizinduka na kujipata akiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti baada ya kuthibitishwa kwamba alikuwa amefariki na madaktari watatu, vyombo vya habari Uhispania vinasema.

Gonzalo Montoya Jiménez alikuwa anazuiliwa katika gereza moja jimbo la Asturias na alizinduka saa chache tu kabla yake kufanyiwa upasuaji wa kubainisha chanzo cha kifo chake.

Mwili wake tayari ulikuwa umechorwa alama tayari kwa upasuaji.

Kwa sasa, amewekwa chini ya uangalizi wa madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Oviedo.

Mmoja wa jamaa zake ameambia gazeti la La Voz de Asturias kwamba Montoya "alikuwa na alama ya kufanyiwa upasuaji, tayari kupasuliwa".

Inadhaniwa kwamba hicho kilikuwa kisa cha hali iitwayo 'catalepsy' duru katika hospitali hiyo zimeambia runinga ya Telecinco ya Uhispania.

Catalepsy ni hali ambapo ishara muhimu za uhai kwenye mwili wa binadamu hufifia kiasi cha kutoweza kutambulika.

"Kifo" chake kilikuwa kimethibitishwa na madaktari watatu gerezani ambao waliagiza mwili wake upelekwe kwenye ufuo kwa uchunguzi zaidi.

Mwili huo ulipelekwa ufuo wa Taasisi ya Matibabu ya Kisheria katika makao makuu ya jimbo Oviedo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad