Mkuu wa Genge la Yazuka la Japan Akamatwa Thailand

Mkuu wa Genge la Yazuka la Japan Akamatwa Thailand
Polisi wamekamata mkuu wa genge la Yazuka la nchini Jopan ambaye amekuwa mafichoni kwa miaka 15 baada ya picha za chale zake (tattoo) kusamba katika mtadao wa Facebook.

Shigeharu Shirai analaumiwa kwa kumuua mshindan wake kwenye genge hilo mwaka 2003.

Picha za mtoro huyo wa umri wa miaka 74 zilichukuliwa na mtu mmoja nchini Thailand ambaye hakufahamu yeye ni nani.

Magenge ya Yazuka yamekuwa miongoni mwa jamii nchini Japan kwa karne kadhaa na wanakadiriwa kuwa na wanachama 60,000.

Licha magenge hayo kutokuwa haramu, asilimia kubwa ya pesa zao hutokana na kucheza kamari, ukahaba, ulanguzi wa madawa ya kulevya na udukuzi wa mitandao.

Wakati picha hizo zilisambaa mitandaoni, zilivutia polisi wa Japan walioombaa akamatwe.

Polisi walimkamata kwenye mji wa Lopduri kaskanizi mwa Bangkok na atasafirishwa kwenda Japan kukabiliana na mashtaka ya mauaji.

Kulingana na polisi nchini Thailand, alikiri kuwa yeye ni mwanachama wa Yazuka lakini hakukiri kuwa alihusika kwenye mauaji ya mwaka 2003. Alitorokea Thailand mwaka 2005.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad