Msanii wa muziki wa Hip Hop, Moni Centrozone amedai kwamba Roma Mkatoliki hana mchango wowote katika maisha yake ya muziki kama watu wanavyofikiria.
Rapa huyo kutoka Dodoma, amesema kwamba hawezi kumzungumzia Roma kwa jinsi yoyote kwenye sanaa yake na hata kolabo watu wanayofikiria kuwa ilimpa msaada wa kumtambulisha wanakosea kwani haijam[patia lolote zaidi ya dhahama.
Majibu hayo ya ku-‘panick’ yaliyotolewa na Moni yallikuja baada ya kuulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho kama yeye na Country Boy wameamua kuanzisha muungano waliouita (MoCo) ili kushindana na muungano wa ROSTAM unaoundwa na Roma na Stamina na kudai yeye hashindani na watu hao bali yupo kwenye muziki kwa ajili ya kushindana na wasanii.
Moni ameendelea kusema mtu pekee ambaye anayemkumbuka na hawezi kumsahau katika sanaa yake miaka yake yote ni Marehemu Langa kwa kuwa ndo msanii ambaye aligundua kipaji chake na kumchukua kutoka kijijini kisha kumleta mjini kwa ajili ya kurikodi nyimbo na mapaka leo watu wanamtambua.
“Who is Roma kwenye maisha yangu. Mimi simfahamu na wala hajawahi kuntoa kwenye muziki kama jinsi watu wanavyoodhani. Mimi namjua Langa aliyenichukua uswahilini kwetu na kunileta mjini. Sipendi kutajiwa majina ya watu wasio na umuhimu na mimi” alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Mbali na hayo Moni amesema kwamba kundi lao MoCo’ haliwazuii kufanya nyimbo zao binafsi kama ‘solo artist’ na kusema kundi lao limewaunganisha ili kuweza kuleta changamoto kwa wasanii wote ambao wanafanya mziki sawa na wakwao na hawajamlenga kundi wala mtu yeyote.
Mapema mwaka jana Moni alimshirikisha Roma wimbo wake ambao ulimtambulisha zaidi kwenye ‘game’ ya Bongo kisha kumpatia mashabiki kibao na baadae mahusiano yao yakaonekana kuingia dosari pale mwezi Aprili wasanii hao walipotekwa na watu wasiojulikana kisha kuachiwa baada ya siku tatu na baada ya miezi kadhaa Roma akaachia wimbo aliouita ‘Zimbabwe’ ambao ulipata mapokeo makubwa na baadaye Moni kukasirika kwamba kwa nini Roma ameamua kutumia Idea ya kutekwa kwao na kufanya kama tukio hilo lilimtokea yeye binafsi na kumbe liliwapata watu wanne. (Roma, Moni