Moto uliowaka usiku wa kuamkia leo katika eneo la kijiji Langata, Nairobi nchini Kenya umeteketeza nyumba zao na kuwaacha bila nyumba za kulala.
Moto huo ambao chanzo chake bado hakijabainika ulizuka mwendo wa saa mbili jioni na kuenea kwa haraka.
Magari ya kuzima moto ya baraza la jiji yalifika baadaye, lakini wakazi waliwalaumu maafisa hao wa serikali kwa kuchelewa kufika eneo la mkasa.
Moto huo baadaye ulizimwa, ingawa moshi bado ulikuwa unafuka katika baadhi ya maeneo asubuhi.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Kukabiliana na Majanga anayeangazia mawasiliano Bw Pius Masai aliambia gazeti la kibinafsi la Nation kwamba walilazimika kuomba usaidizi zaidi.