Mtulia Afunguka Kuhusu Uamuzi Wake wa Kuhama Chama "Nimefanya Maamuzi ya Kiume"

Mtulia Afunguka Kuhusu Uamuzi Wake wa Kuhama Chama "Nimefanya Maamuzi ya Kiume"
Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Maulid Said Mtulia amesema amefanya maamuzi ya kiume ya yeye kuhamia chama hicho kwa sasa kwa maana wapo wengi wanataka kufanya hivyo lakini wameshindwa kwa madai wanasubiri kulipwa kiunua mgongo.


Mtulia ameeleza hayo wakati alipokuwa anaendelea kujinadi kwa wananchi wa jimbo la Kinondoni ambalo hapo awali alikuwa analishikilia yeye kupitia chama chake cha CUF kabla ya kujivua uanachama wake na kuenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kuijenga nchi.

"Kujiuzulu Ubunge sio mchezo, nimefanya maamuzi ya kiume maana kuna wenzangu wengine mpaka sasa hawawezi kutoka kwa sababu wanasubiri kiunua mgongo. Sasa kijana kama mimi nikae pale nisubirie kiunua mgongo hivi kweli ntaweza kuishi kwa kusubiri kiunua mgongo", alisema Mtulia.

Aidha, Mtulia amesema amejinusuru kwa mengi kukihama chama chake cha awali ili aweze kuwapigania wananchi wa jimbo hilo kwa maana hapo awali alikuwa anashindwa kuyafanya majukumu yake vizuri kutokana na mgawanyiko ndani ya chama chao.

"Wenzangu Wabunge 10 walifukuzwa uanachama CUF hamkujua, mlisubiri nifukuzwe au mna roho mbaya na mimi. Hivi nilipo hapa nimeruka kwa kujinusuru nashukuru nipo salama na nimesimama tena kwa wana kinondoni ninaomba kugombea Ubunge nyie mnanuna kitu gani au huo ndio usaliti. Lakini jambo jingine mimi nimekuja CCM kwa sababu nampenda Magufuli balaah", aliuliza Mtulia.

Pamoja na hayo, Mtulia aliwashangaza baadhi ya watu kwa kusema ametumikia Ubunge ndani ya miaka miwili na kushiriki vikao vyote vya Bunge lakini hakuweza kuwa na namba ya Rais Magufuli.

"Leo ninawaambia siri yangu, nilivyokuwa Mbunge miaka miwili namba ya Rais Magufuli sikuwa nayo lakini sasa namba ninayo. Hivyo wanakinondoni mnataka nini kama mnataka maendeleo ndio haya", alisisitiza Mtulia.

Kwa upande mwingine, Mtulia amewaambia wananchi wa Jimbo la Kinondoni endapo watamchagua yeye katika chaguzi hizo za marudio zilizopangwa kufanyika mapema Februari 17 mwaka 2018 basi watakuwa wametengeneza daraja la kujipatia maendeleo.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bilion moja hii mnayochezea ingejenga hispitali ngapi? kuna mama anakata roho kule kijjijini sababu miundo mbinu ya kujifungulia si salama
    kuna mwananchi kule kijijini anagombea maji kwenye dimbi na simba ngombe mbwa
    kuna mtoto kakaa juani kule kijijini tangu asubuhi anasomea juani mvua ikinyesha ni likizo
    kuna raia hawana ajira wala hawajui la kufanya wewe ni mwanaume wa kiume kweli
    kwanini usingepambana na yote haya ukiwa palepale ...chama kilekile bila kuumiza wengine?
    utawalipa nini wale wanachi waliokimbizana na polisi wakati ukiwa cuf wakakupigania ama kweli wewe ni mwanaume.........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad