Muslim Hassanali Baada ya Kuingia CCM Ajipachikia Nafasi ya Kuwa Mshauri wa Rais

Muslim Hassanali Baada ya Kuingia CCM Ajipachikia Nafasi ya Kuwa Mshauri wa Rais
Aliyewahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Ilala kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2015, Muslim Hassanali amejipachika nafasi ya ushauri wa serikali ya Rais Magufuli kwasababu nafasi hiyo haihitaji kuteuliwa.

Akizungumza leo katika ukumbi wa Checkpoint eneo la Pugu jijini Dar es salaam, katika maandalizi ya kumpokea akitokea upinzani kwenda CCM leo ambapo amesema kuwa hajaingia katika chama hicho kutafuta mali.

“Naomba niwaweke wazi kuwa sijpewa na sijahaidiwa nafasi yoyote na serikali au CCM, nafasi nimeitafuta mwenyewe na cheo changu kuanzia leo naomba nikiweke wazi Mh. Mwenyekiti cheo changu ni mshauri wa serikali ya Magufuli nani ya nchi hii, kuwa mshauri hakuhitaji kuteuliwa nimejiteua mwenyewe,“ amesema Muslim Hassanali .

Aidha Hassaniali aliongeza kuwa “Haikuwa kazi rahisi kuchukua maamuzi ya kuihama CHADEMA na kujiunga CCM, Ila imebidi niweke maslahi yangu binafsi pembeni na kujiunga CCM ili nipambanie nchi yangu“.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad