Mwakyembe Ashtushwa na Vitendo vya Uonevu kwa Waandishi wa Habari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Harrison Mwakyembe ameshtushwa na malalamiko ya wadau wa soka kuhusu vitendo vya unyanyasaji na uonevu kwa Waandishi wa Habari wanaoripoti matukio ya michuano ya soka Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Waziri Mwakyembe amelitaka Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) kuchunguza tuhuma hizo kujua kama kuna ukweli juu ya vitendo hivyo ambavyo vimejitokeza kwenye michezo miwili ya Ligi daraja la kwanza iliyochezwa Desemba 30, 2017 kati ya Dodoma FC vs Alliance ya Mwanza, na Pamba FC vs Biashara ya Musoma.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Picha inaonyesha km museveni au ndo Mwakyembe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad