Mwenyekiti wa zamani wa Simba Mzee Hassani Dalali amewashukia wachezaji mastaa wa klabu hiyo kwamba wanatakiwa kujituma na kupambana kwa ajili ya klabu ili ipate ubingwa, hakuna mchezaji ambaye ni mkubwa kuliko klabu ndio maana wamesajiliwa.
Dalali amsema hakuna kitu kingine ambacho wanachama wa klabu hiyo wanahitaji zaidi ya ubingwa ambao wameukosa kwa muda mrefu.
“Hata kama jina lako kubwa Simba ni kubwa kuliko wewe ndio maana imekusajili, onesha uwezo wako sisi tunahitaji ubingwa hakuna kitu kingine. Katika miaka nane tangu nimeondoka madarakani tumechukuwa ubingwa mara moja (2011/12) wakati Ismail Aden Rage akiwa madarakani lakini ubingwa ule si kwa kumfunga mtu, wamecheza Mtibwa na Azam, kafungwa Azam Simba kawa bingwa wakati yupo nyumbani kalala.”
“Timu ya Mbao kuna kijana mdogo anaitwa Imran Kalman ameidhamini Mbao kawapa basi anatoa pesa nyingi katika timu, angalia Mbao wanavyocheza wanajituma, wanaona thamani ya timu yao walicheza na Simba 2-2 Yanga kaingia kafungwa iweje sisi Simba? Wachezaji wanashindwajie kupafomu uwanjani? Wanachama wanaumia, mimi naomba wachezaji wa Simba kama kuna tatizo waweke wazi kwa viongozi, wazee au wadhamini wa klabu wakaseme kama wanadai au viongozi.”