Mzee Majuto Afunguka Alivyokosa Kitanda Muhimbili

Mzee Majuto Afunguka Alivyokosa Kitanda Muhimbili
Muigizaji Staa ndani ya Bongo Movie Mzee King Majuto  ameeleza ilivyokuwa mpaka akakosa kitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na ugonjwa unaomsumbua kwa sasa.

Majuto amesema ili mbidi arudi kulala Vingunguti saa nane usiku baada ya kukosa kitanda katika vyumba VIP ambapo wao walihitaji, pia ameeleza kuwa anaugua Tezi Dume na ameshafanya vipimo  ila anatakiwa arudi siku ya Jumanne kwa ajili ya kuangalia namna ya kupata matibabu zaidi.

“Ilikuwa nipumzike ila tulihitaji VIP sasa sijui tatizo lilikuwa nini au ndo haya mambo ya Ki-TZ mpaka uonyooshe mikono, askari wa pale alibishana na mke wangu mwisho akasema hakuna chumba ili Saa nane usiku tufanye utaratibu wa kurudi nyumbani, tatizo ni tezi dume,”-King Majuto

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad