Nabii Akamatwa na Dawa Haramu Zambia

Nabii Akamatwa na Dawa Haramu Zambia
Mchungaji Isaac Amata (42) wa Nigeria, ambaye mwaka 2016 alimtabiria ushindi Rais Edgar Lungu amewekwa ndani akituhumiwa kusafirisha kilo 26.29 za dawa zilizopigwa marufuku.
Mchungaji huyo anayefahamika pia kama Nabii alikamatwa na maofisa wa kupambana na dawa za kulevya Jumatano alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, amesema msemaji wa Tasisi ya Kupambana na Dawa za Kulevya Theresa Katongo.
Katongo alisema mchungaji huyo aliyekamatwa baada ya kuwasili akitokea Nigeria alikuwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
Kwa sasa, msemaji huyo alisema anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani muda wowote.
Dawa alizokamatwa nazo ni aina ya ephedrine, ambazo hutumika kusisimua misuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad