Ndoa ya Sasha Yaota Mbawa " Suala la Ndoa Halipo Tena na Mahari Sirudishi"

Ndoa ya Sasha Yaota Mbawa " Suala la Ndoa Halipo Tena na Mahari Sirudishi"
MWANADADA mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Sasha Kassim ambaye alikuwa anatarajia kuolewa siku chache zijazo amesema kuwa, ishu hiyo haipo tena na mahari hairudishwi.

Akizungumza na Star Mix, Sasha alisema mwanaume huyo aliyemtaja kwa jina moja la Boniphace amejikuta akishindwa kuendelea naye sababu ya wivu, amekuwa akimuonea wivu picha anazoposti mtandaoni na kumtaka asitumie mitandao ya kijamii, jambo ambalo hayupo tayari kukubaliana nalo.

“Suala la ndoa halipo tena, yeye alinipata mtandaoni cha ajabu ananikataza kutumia mitandao nimeona sitoweza kuminywa uhuru wa maisha yangu kwa kiasi hicho, hivyo uchumba umevunjika na mpango wa kurudisha mahari haupo kabisaaa,”alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad