Papa Francis Aozesha Wanandoa Kwenye Ndege

Papa Francis Aozesha Wanandoa Wakiwa Kwenye Ndege
Kwa taratibu za ndoa za Kikatoliki ni vigumu kuzivunja hadi kuozeshwa na Papa, tena kwenye ndege. Lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa Alhamisi baada ya Papa Francis kuwaozesha wahudumu wawili katika sherehe fupi umbali wa futi 36,000 angani.

Maofisa wa Vatican walisema jana kwamba hiyo ilikuwa mara ya kwanza katika historia papa kuwapa sakramenti ya ndoa wanandoa kwenye ndege ya papa.

Tukio hilo lilianza wawili hao, Paula Podest Ruiz na Carlos Ciuffardi Ellorriaga walipokuwa wakizungumza na kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani wakiwa wamekaa karibu yake na wakipiga picha. Ndege ilikuwa inamsafirisha Papa kutoka Santiago kwenda mji wa Kaskazini wa Iquique.

Papa Francis aliwauliza ikiwa ni wana ndoa nao walimjibu kwamba ndoa yao ilipangwa mwaka 2010 lakini iliahirishwa kutokana na tetemeko la ardhi kuikumba Chile na kuharibu kanisa walilopanga kufungia.

Maisha ya wapenzi hao waliokutana kazi yalisonga mbele na wakapata watoto wawili Rafaela, 6, na Isabela, 3. Walioana serikalini na walikuwa na vyeti vya uthibitisho lakini hawakuwa wameoana kanisani.

Paula Podest Ruiz, mwenye umri wa miaka 39, na Carlos Ciuffardi Elorriga, mwenye umri wa miaka 41, waliozwa na Papa katika siku ya tatu ya ziara yake ya Amerika Kusini wakiwa angani ndani ya ndege ya shirika la LATAM.

Papa Francis alitarajiwa kwenda Peru, ambako atakutana na watu wa asili watakaomueleza jinsi uchimbaji wa dhahabu unavyoendelea kuharibu maeneo makubwa ya msitu wa Amazon nchini humo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad