Pius Msekwa: Ni Vigumu Kuzuia na Kuondoa Rushwa

Pius Msekwa: Ni Vigumu Kuzuia na Kuondoa Rushwa
MWANASIASA mkongwe nchini, Pius Msekwa, amesema ni vigumu kuzuia na kuondoa rushwa nyakati za uchaguzi kwa sababu za ugumu wa kimazingira ya ushahidi kwani mara nyingi vitendo hivyo hufanywa na watu waliokubaliana.



Msekwa ambaye ameshika nafasi mbalimbali za uongozi nchini ikiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameyasema hayo leo nyumbani kwake, Oyster Bay Jijini Dar katika mahojiano maalum na Global TV Habari na kuongeza kuwa zinahitajika juhudi za kipekee ili kuondoa tatizo la rushwa katika uchaguzi.

“Siyo rahisi kuizuia rushwa wakati wa uchagzui, kwanza mtoaji na mpokeaji wote wanakubaliana, utawazuiaje? Huwezi kuzuia rushwa kwa matamko, unahitaji kutunga sheria, watuhumiwa wakikamatwa uwe na ushahidi wa kuithibitishia mahakama,” alisema Mzee Msekwa.



Taifa limeshuhudia juhudi kubwa zimeoneshwa na Rais wa jamhuri ya Muunganowa Tanzania kuhakikisha anawadhibiti watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwakuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikishwa mahakamani.

Hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) Taifa, Sadifa Juma alikamatwa na TAKUKURU mjini Dodoma kwa tuhuma za rushwa na kufikishwa mahakamani wakati wa mchakato uchaguzi wa viongozi wa  UVCCM.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad