Polisi Kuchukua Hatua Hizi Endapo Utakutwa Umevaa Nguo Fupi

Jeshi la Polisi limetangaza kufanya msako kwa watu wanaovaa nguo zisizo na heshima, kulingana na maadili ya Tanzania na kuwafikisha mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo wakati akitoa taarifa ya usalama kwa mwaka 2017, alisema hivi sasa kuna wimbi la mavazi yasiyo sahihi wanayovaa baadhi ya watu.

Alitaja baadhi ya nguo hizo kuwa ni fupi, zinazoonyesha nguo za ndani na suruali za kubana maungo.

“Hizi nguo hazipendezi na siyo maadili yetu, mnaiga wenzenu wananyovaa kwa sababu ya hali ya hewa ya kwao, sasa tunatangaza msako mwaka huu na tutakayemkamata tunamchukua hivyo viyo hadi mahakamani bila kumpa nguo ya kujifunika ili ndugu zako wakuone,” alisema kamanda Mkumbo.

Mkumbo aligusia pia kuongezeka kwa matukio ya kubaka na kulawiti tofauti na matukio mengine ambayo yamepungua kutokana na jitihada za Jeshi hilo kutoa elimu kwa wananchi.

Alisema matukuo ya kubaka kwa mwaka 2016 yalikuwa 144 na mwaka 2017 yaliongezeka hadi kufikia 149, huku makosa ya kulawiti yakiongezeka toka 58 mwaka 2016 hadi 62 mwaka 2017.

Alieleza sababu kubwa ya kuongezeka kwa makosa hayo ni uwepo wa mila potofu na imani za waganga wa kienyeji pamoja na ukosefu wa elimu.

Aidha alisema ni vyema kila Mtanzania akafahamu kuwa vitendo hivyo havikubaliki na adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 au kifungo cha maisha jela.

Mkumbo alisema wakati matukio ya ubakaji na kulawiti yakiongezeka , matukio ya kihalifu yamepungua kutoka 2,817 mwaka 2016 hadi kufikia 1,963, mwaka 2017. ambapo jumla ya makosa 854 yamepungua sawa na 17.9% na kuwaomba wananchi kuendelea kulinda amani ya mkoa huo ili waweze kupata maendeleo ya kiuchumi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad