Polisi yatumia Helikopta Kuangalia Kusalama Dar

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema wanatumia helkopta ili kuangalia maeneo ambayo yamepata madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kaimu kamanda wa polisi kanda kanda hiyo, Benedict Kitalika akizungumza leo Jumatatu amesema kutokana na mvua zilizonyesha jeshi hilo limeamua kutumia helkopta hiyo ili kujua ni maeneo gani yameathirika.

"Kuanzia sasa hivi tumeanza kuangalia sehemu mbalimbali kwa kutumia helkopta hivyo tutawajuza baadaye kama kuna madhara yametokea kutokana na mvua hizi zinazoendelea," amesema Kitalika.

Pia amewataka madereva wanaotumia barabara ya Morogoro wasipite Jangwani kutokana na maji yanayopita juu ya daraja.

Amesema njia wanayotakiwa kupita wakifika Magomeni usalama wapite barabara inayotokea Ilala na  barabara inayoelekea Kinondoni.

"Barabara inayotokea Kigogo haina madhara hivyo madereva waitumie isipokuwa ile ya Jangwani haipitiki," amesema Kitalika

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad