Raila Odinga: Siogopi Kuwekewa Vikwazo

Raila Odinga:  Siogopi Kuwekewa Vikwazo
 Raila Odinga, kiongoni wa muungano wa upinzani amesema “haogopi kuwekewa vikwazo” vyovyote kutokana na mkakati wake wa ‘kula kiapo cha kuwa rais wa watu’ katika sherehe zilizopangwa Jumanne ya Januari 30, 2018.

Odinga alisema amepigiwa simu nyingi na amepokea vitisho kutoka kwa mabalozi mbalimbali na “marafiki wa nje” wakimtaka kutoendelea na mpango wake wa kuapishwa, lakini akasema ataendelea hata kama hiyo itamgharimu kwa kutosafiri nje.

Kiongozi huyo wa muungano wa National Super Alliance (NASA) alisema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake wa mkoa wa Nyanza.

“Marafiki zangu wa ughaibuni na mabalozi wamekuwa wakinisihi nisile kiapo. Kunipa onyo juu ya kuwekewa vikwazo na haki yangu ya kidemokrasia kuchafuliwa, lakini sina mpango wa kusafiri nje, nanajibiisha kupambana dhidi ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi katika nchi,” alisema Odinga.

Odinga ameendelea kusisitiza kwamba alishinda uchaguzi wa Agosti 8, 2017 ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu baada ya Nasa kufungua kesi kupinga Tume Huru ya Uchaguzi kumtangaza Uhuru Kenyatta kama mshindi.

Odinga na Nasa walisusia uchaguzi wa marudio ulioamriwa na Mahakama Kuu ambao Uhuru alishinda kwa asilimia 98. Uhuru aliapishwa kuwa rais lakini Nasa alikataa kuitambua serikali yake badala yake wakaanzisha mpango wa kuunda serikali itakayoongozwa na Odinga kama rais wa watu.

Serikali ya Uhuru imetoa onyo kali juu ya madhara makubwa yanayoweza kumkuta “yeyote atakayejiingiza kulivuruga taifa”. Wito wa majadiliano kati ya serikali na upinzani haujazaa matunda.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad