Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse.
Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari.
''Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa M arekani pekee,taarifa iliotoka katika msemaji wa Ikulu Raj Sha ilisema.
Iliendelea: Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu na kuingiliana na raia wa taifa letu.
Kamwe hatakubali mkakati wa muda mfupi ulio hafifu na hatari ambao unahatarisha maisha ya raia wa Marekani, mbali na kutowaruhusu wahamiaji wanaotaka maisha mazuri Marekani ijapokuwa kupitia njia halali.
Waandamanaji wanaopinga chuki ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji
Image caption
Waandamanaji wanaopinga chuki ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji
Matamshi hayo ya rais Trump yanajiri huku wabunge kutika vyama vyote wakimtembelea kupendekeza mpango wa wahamaiji usiopendelea upande wowote.
Seneta wa Democrat Richard Durbin alikuwa akizungumza kuhusu vibali vya muda wa kuishi vinavyotolewa kwa raia wanaotoka katika mataifa yaliokumbwa na majanga, vita ama milipuko ya magonjwa, vilisema vyombi vya habari.
Kulingana gazeti la Washington Post , bwana Trump aliwaambia wabunge kwamba Marekani badala yake inachukua wahamiaji kutoka Norway, ambayo waziri wake mkuu alimtembelea rais Trump siku ya Jumatano.
Seneta Lindsey Graham, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republian kutoka Carolina Kusini pia alikuwa katika mkutano huo lakini hakuweza kuzungumzia kuhusu matusi hayo yaliotolewa na rais Trum.
Gazeti la The New York Times liliripoti miaka mitatu iliopita kwamba bwana Trump alisema kuwa raia wa Haiti wote wana ''ukimwi'' wakati wa mkutano wa mwezi Juni kuhusu wahamiaji.
Na kufuatia matamshi hayo rais Trump hakusazwa katika mitandao ya kijamii.
Elijah Cummings, mbunge wa Democrat katika eneo la Maryland alichapisha ujumbe katika mtandao wa twitter akisema: Nayashutumu matamshi hayo yasiosameheka na yanayoshusha hadhi ya afisi ya rais.
Mbunge mwengine mweusi kutoka chama cha Democrat. Cedric Richmond, alisema matamshi ya bwana Trump ni dhihirisho tosha kwamba sera yake ya kuliimarisha taifa la Marekani ni sawa na kulifanya taifa la Marekani kuwa la watu weupe pekee.
Mia Love, raia wa chama cha Republican katika eneo la Utah ambaye pia ni mbunge wa pekee mwenye mizizi ya Haiti nchini Marekani amemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa maneno hayo yalio na chuki na yenye kugawanya watu.
Muungano unaopigania haki za watu weusi NAACP ulimshutumu rais Trump kwa kuzidi kuegemea katika ubaguzi wa rangi.
Lakini Ikulu ya Whitehouse imepuuzilia mbalia shutuma hizo zinazomkabili rais.
Afisa mmoja wa Trump alinukuliwa na chombo cha habari cha CNN akisema: Ijapokuwa hili litawakasirisha watu wa Washington, wafanyikazi wanadhani kwamba matamshi hayo yanatokana na mizizi yake, sawa na matamshi yake dhidi ya wachezaji wa NFL waliopiga goti wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa taifa.
Msemaji wa ubalozi wa El Salvador mjini Washington alikataa kuzungumzia kuhusu matamshi hayo.
Rais Trump Ayatusi Mataifa ya Afrika Haiti na El Salvador
1
January 12, 2018
Tags
Sisi Waafrica wacha tuendelee kutukanwa na wazungu. Sisi wenyewe hatujasamini na mifano ipo hai mingi tu. Wahenga wanasema ukihitaji staha lazima uanze kujiekea staha wewe mwenyewe kwanza. Kwa mfano wamerekani weusi wametengezewa picha kana kwamba ni watu hatari na wakorofi lakini ukweli ni kwamba sio hivyo. Wamerekani weusi wana hasira iliojengeka kutoka kizazi hadi kizazi kutokana na maonevu, ubaguzi na dharau na kubwa zaidi wanahisi kuna mifumo fukani fulani hivi iliwabana au inaendelea kuwabana kushindwa kufikia fursa za kiuchumi zaidi. Ni nadra kumuona Mmarekani mweusi akijokomba kwa mzungu kwa sababu wameyaishi maisha yao na kuwaelewa hasa jinsi gani wanavyouabudu ubaguzi hata kama anajifanya kucheka na wewe. Hakuna jinsi kwa mataifa ya Africa isipokuwa kuboresha hali ya mataifa yao kiuchumi. Ndipo pale ninaimani kwa watanzania wengi au niseme waafrica tunaoshi nje ya Africa ambao uzalendo wa uafrica upo kwenye adamu tunaumizwa sana kuona kuna watu au wanasiasa wameamua kwa makusudi kabisa kupambana na Maghufili kwa kweli wanafanya makosa makubwa sana. Kitendo cha Magufuli kutosafiri kwenda nchi yeyote ya Ulaya au Marekani na kujikita zaidi katika ujenzi wa nchi yake ni ushahidi tosha yakuwa Magufuli ni miongoni mwa viongozi au waafrica wachache wanaojitambua. Ujenzi wa nchi za kiafrica hasa kiuchumi ili kufikia viwango vya kumkomboa muafrika kutokana na umasikini mara nyingi umekuwa ukikatizwa na matatizo kadhaa wa kadhaa lakini tatizo kubwa zaidi ni kukosekana kwa viongozi wenye uzalendo wanaoweka maslahi ya nchi kwanza. Kumpata kiongozi wa dhati anaekuwa mkali kwa viongozi wengine wa nchi anaowaongoza kuhakikisha kila kiongozi mwenye dhamana anaweka maslahi ya nchi Kwanza ni jambo liloshindikana Africa hata wanapotokezea viongozi wa namna hiyo huwa hawadumu kutokana na mafigisu wanayoyapata kutoka ndani na hata nje ya Africa na wakati mwengine inapelekea hata kupotezwa maisha yao kikatili. Kwa hivyo wacha Waafrica tutukwane kwa sababu ni wapumbavu. Leo Tanzania tunakiongozi mfano wa padre kwa upole watu lakini tunashuhudia watu hawalali wanahangaika kila jinsi namna ya kumchafua mpaka nje ya nchi. Kutokana na matatizo ya kiuchumi na ya kiuongozi tuliokuwa nayo Tanzania na kazi wanayoiendelea kuifanya Magufuli Tanzania we are supposed to proud of him loudly. Kasoro chache tena zinazokuzishwa zaidi na wanasiasa hazikupaswa kuwa ndio sababu za kumjengea Magufuli na serikali yake mazingira magumu ya kuijenga hii nchi. Magufuli aliposema nchi yetu ipo katika vita ya uchumi yeye ni amiri jeshi mkuu hakujisemea tu, tulitarajia kuona kila mtanzania anapambana, anafocus kwenye ujenzi wa uchumi wa taiafa letu kwanza na kuweka mambo ya siasa pembeni. Lakini unaona kabisa wanasiasa wetu wanahangaikia na kulilia viwanja vya kufanyia mikutano ya hadhara badala ya kulilia kushirikishwa katika ujenzi wa uchumi japo kumuomba muheshimiwa raisi wakati huu wa sera ya viwanda na wao wapinzani wakawa na kiwanda cha mfano. Lakini hapana wanatumia muda mwingi kulilia matangazo ya t.v. ili wapate muda wa kuitukana serikali ni vitu vya kushangaza kabisa na bado kuna watu wanawaunga mkono. Ndipo nnaposema sisi waafrica ni wapumbavu wacha tuzarauliwe. Kama Maghufili angelikuwa kiongozi wa kizungu jinsi anabyolipigania taiafa lake basi akina Zito Kabwe tayari walishamuandkia vitabu vya utukufu. Kuna tofauti gani ya kauli chafu ya raisi wa Marekani na kauli ya Tundu Lisu kumuita Raisi wa Tanzania SKUNK au Ngawa? Utaona kabisa licha ya maafa yaliyompata Tundu Lisu lakini ni mtu aliedhamiria Shari juu ya watawala wa nchi tangu mwanzoni kabisa ni kwa bahati mbaya kwa taifa na Lisu kumfika yaliomfika lakini sidhani ni sahihi kwake kuendeleza kampeni ya kuikomoa na kuipaka matope Tanzania zaidi ni kujipaka matope yeye mwenyewe binafsi.
ReplyDelete