Mkali wa R&B na mshindi wa tuzo mbalimbali, Rama Dee, aliyetamba na ngoma kali kama ‘kuwa na subira’, ‘Kipenda roho, na nyinginezo kibao, ameamua kufungua mwaka 2018 kwa kitu cha tofauti kabisa kinachokwenda kwa jina la ‘FURAHA YETU’.
Wimbo huo wa FURAHA YETU wenye staili kali na ya kitofauti unaotarajiwa kutoka rasmi ijumaa hii ya Januari 5, Rama Dee anasema alivyoangalia mahusiano ya watu jinsi yanavyoenda ndipo alipata wazo lake.
“Idea ya wimbo wa “tuwe na furaha” ilikuja baada ya kuona watu wengi kwenye mahusiano hawana furaha, si kwamba hawapendani no ila hawajui kama wanaishi kwa furaha kwa kuangalia na kuamini vitu vilivyo mbele ya camera”. Amesema Rama Dee
Pia kutokana na experience ya kuzungukwa na marafiki wanaopenda kuchukia kila kitu unachofanya, nako kulifanya wazo la wimbo huo kuibuka
“Lakini pia, niligundua marafiki wengi hawana furaha wana-hate kila kitu kizuri wakifanyacho watu wengine, hawajiamini, hawakubali kuwa wapo kwenye ulimwengu wa furaha”. Kasema Rama Dee
Rama Dee ambaye ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 3 akitanguliwa na dada na kaka mmoja, anasema lengo la kutumia staili hii ya twist ni kutimiza moja ya ahadi aliyowahi kumhaidi mama yake
“Marehemu Mama yangu alipenda sana muziki wa aina hii (twist), pia niliwahi kumwambia siku moja hii style nitaiweka kiujana ili iendelee kupendwa”. Amesema Rama Dee
Wimbo huo uliofanyika katika studio za ‘Hometown studio’, Producer akiwa yeye mwenyewe kwa kushirkiana na Elly Da Bway, Rama Dee anaamini wimbo huu sio kwaajili ya kucheza tu, bali ni maalum kwa kuwakumbusha watu kuwa maisha ni mafupi na tunahitaji kuishi kwa furaha.